Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara wajipanga kuwekeza sekta ya viwanda
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara wajipanga kuwekeza sekta ya viwanda

Spread the love

WAFANYABIASHAFA wakubwa nchini, wamejipanga kuendelea kujenga viwanda vikubwa na vidogo katika maeneo mbalimbali nchi ili kuongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa Taifa, anaandika Moses Mseti.

Wamesema licha ya baadhi ya watu kudai Tanzania sio sehemu sahihi ya kuwekeza, lakini wao wameona kuna fursa ya kuwekeza husasani katika awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli hivyo ni muda muafaka wa kuwekeza ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza leo jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Victoria Moulders, Altaf Mansoor, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Sigara kinachofahamika kama Phillip Morris kilichopo Morogoro, amewataka watanzania na wafanyabiashara wengine kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini kwa kuwa tayari mazingira sahihi ya kufanya biashara yameboreshwa.

Mansoor ambaye pia ni Mkurugenzi wa kiwanda cha Mansoor kinachojishughulisha na uuzaji wa mafuta ya taa na dizeli, amesema kama mfanyabiashara mzawa yupo tayari kuwekeza nchini kwake kwa kuwa Serikali inathamini wawekezaji wa wazawa.

“Mazingira ya kuwekeza nchini sasa hivi ni mazuri na kuna watu wachache wanapotosha kwamba Tanzania siyo sehemu sahihi baada ya kuona biashara zao wanazozifanya haziendi vizuri,” amesema Mansoor.

Mkurugenzi wa kiwanda cha Victoria Moulders, Manjit Sandhu, amesema miradi ya viwanda vya kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2001, ambapo kiwanda cha mwanza kitakuwa kinatengeneza matenki ya maji, mabomba ya maji, viti vya plastiki, ndoo, mabeseni na madiaba.

Pia amesema baada ya kiwanda hicho kuanzishwa na kitakachokuwa kinauza bidhaa zake nje ya nchi ikiwemo DR Congo, Uganda na China, kimeajiri zaidi ya watanzania 500 pamoja na kuchangia katika uchumi wa Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!