June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara vilainishi kudhibitiwa

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za nishati na Maji (EWURA) imeanza kufanya kazi kwa  pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Viwango (TBS) ili kudhibiti wafanyabiashara wa vilainishi  wanaoingiza bidhaa  sisizo na ubora sokoni, anaandika Christina Haule.

Akizungumza na wafanyabiashara wa mafuta leo mkoani Morogoro, Godwin Samuel, Mkurugenzi  Idara  ya  Petrol amesema, wafanyabaishara wengi wa vilainishi wamekuwa wakiigiza bidhaa  zisizo na ubora kwa watumiaji na  hivyo  kupelekea  kuwepo kwa malalamiko.

Amesema kuwa, kanuni za EWURA zinazosimamia biashara ya vilainishi ya mwaka  2014, imeanza kusimamia biashara za vilainishi kwa kuanza kutoa leseni kwa wafanyabiashara na kusajili vilainishi.

Aidha, mkurugenzi huyo amesema kuwa EWURA ina jukumu  la  kudhibiti  sekta  ya Petroli  kiufundi,  kiuchumi na kiusalama, ikiwa ni pamoja na kutoa pia kusimamisha vibali kwa mujibu wa sheria.

Hata  hivyo  mkurugenzi  huyo  amedai kuwa, kazi ya EWURA ni kuwalinda watumiaji, wafanyabiashara  na maslahi ya serikali na kutokana na athari zinazoweza kujitokeza katika biashara ya vilainishi.

Amewataka wafanyabiashara wa mafuta kujenga tabia ya kupenda kujifunza sheria za mafuta ili kuwafanya kuzingatia misingi ya sheria za biashara ya mafuta, gesi na vilainishi .

 

error: Content is protected !!