July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara magogo walia na serikali

Magogo yakiwa tayari kwa kusafirishwa baada ya kuvunwa

Spread the love

WAFANYABIASHARA wa mbao na magogo mkoani Lindi na Tanga wameiomba serikali kupunguza utitiri wa kodi. Anaandika Jimmy Mfuru, aliyekuwa Kilwa … (endelea).

Ni kutokana na usumbufu unaochochea baadhi ya wafanyabiashara hao kufilisika huku wengine wakilazimika kukwepa kodi hivyo kuikosesha serikali mapato.

Wamesema, kuwepo na vituo vingi vya ukaguzi barabarani kumejenga mazingira ya watumishi wa vituo hivyo kuomba rushwa hivyo jitihada zaidi zinahitajika kupunguza vizuizi hivyo ili kuondoa usumbufu.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki katika warsha ya wavunaji na wafanyabiashara wa mbao na magogo iliyofanyika katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na Wilaya za Mkinga na Korogwe mkoani Tanga.

Warsha hiyo iliyoshirikisha zaidi ya wafanyabiasha 40 kutoka mikoa hiyo, iliandaliwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) na  Mfuko wa Dunia wa Kuhifadhi Mazingira (WWF) – Tanzania. 

Ally Kinunga ni Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Mbao Lindi (UWAMBALI), akichangia katika warsha hiyo amesema, kutokana na utitiri wa kodi katika kuvuna rasilimali za misitu,  imekuwa kero na imewalazimu kuvuna kinyemela na kuikosesha serikali mapato. 

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Kinunga amesema, serikali inapaswa kuweka viwango vyenye tija ili isiendelee kupoteza mapato.

Amesema, wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi hasa katika taratibu za uvunaji kwa kuzungushwa hadi kupata leseni za uvunaji kutoka halimashauri na zile za Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Amesema, suala la kugongewa alama ya nyudo  katika magogo (kuhalalisha) kazi inayofanywa na wilaya badala ya vijiji, imesababisha usumbufu na kuwakatisha tamaa hivyo wameomba nyundo hizo zimilikiwe na vijiji ili kupunguza bughuda hiyo.

Mkoani Tanga kwenye Wilaya ya Korogwe mfanyabiashara wa mbao Adamu Mussa amesema, suala hilo la biashara ya mbao liachwe kuingiliwa na wanasiasa.

Ametaka libakie kwa wataalamu ili kupunguza adha katika zoezi la uvunaji na kuwalazimu kutoa rushwa hasa katika upatikanaji wa leseni na kugongewa nyudo ili hali na wajibu wa watendaji hao.

Nae  Faustine Ninga-Mratibu wa Miradi ya Usimamizi Shirikishi wa Maliasili (TNRF) amesema, warsha hiyo kwa wadau hao ni sehemu ya utekelezaji mradi wa miaka mitatu 2014/17 washirika kati ya TNRF na WWF-Tanzania unaofadhiliwa na WWF-Finland na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.

Ninga ameongeza kuwa, malengo mengine ya mafunzo ni kutoa elimu katika mambo ya uwekezaji katika misitu na ardhi nchini Tanzania na kuwafanya wananchi kufaidika na mazao ya misitu kupitia usimamizi shirikishi wa misitu.

Amesema, mafunzo hayo malengo makuu ni mbinu za kutatua migogoro inayohusu  uwekezaji katika misitu na ardhi hasa kuendesha mijadala na wadau mbalimbali na kutafuta mbinu bora za kuendesha mambo ya  uwekezaji.

error: Content is protected !!