Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara kutoa elimu ya Corona minadani
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara kutoa elimu ya Corona minadani

Wafanyabiashara ndogondogo minadani
Spread the love

UONGOZI wa Umoja wa Wafanyabiashara waendao minadani Mkoani Dodoma (UWABIMIDO) umesema kuwa pamoja na kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato lakini wanatoa elimu ya kujikinga na kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Corona kwa wateja wao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Jeremia Magawa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu juhudi ambazo wanazifanya kuhakikisha wanapambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Kiongozi huyo alisema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa afya za watu uongozi umekuwa ukitoa elimu katika minada kwa kushirikiana na viongozi wa afya katika maeneo husika ili kuwaelimisha juu ya kujikinga na ugonjwa huo ambao ni tishio la kidunia.

Magawa alisema wamelazimika kufanya hivyo kutokana na wao kushirikiana na wataalamu wa afya kupewa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ambayo wamekuwa wakipewa mara kwa mara na wataalamu wa afya baada ya kuunda umoja huo na kutambuliwa rasi na uongozi wa Jiji la Dodoma.

Kiongozi huyo alisema kuwa awali kabla wafanyabiashara hao kutokuwa na umoja walikuwa wakifanya biashara zao katika mazingira hatarishi kwa kuwa walikuwa hawatambuliki wala hawajulikani rasmi jambo ambalo lilikuwa likiwafanya kufanya biashara zao katika mazingira hatarishi.

“Kabla hatujawa na umoja huu na hatujatambiliwa rasmi na Jiji tulikuwa hatuwezi kupata elimu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko au isiyokuwa na milipuko kwani tulikuwa tukifanya kazi zetu katika sehemu hatarishi ya barabara ya kumi eneo la independence.

Kutokana na kupatiwa elimu ya kujikinga na maambukizi ya Corona, uongozi wa UWABIMIDO umeamua kutoa elimu kwa jamii wanayoihudumia ikiwa ni pamoja na wao kwa wao kuwa msitari wa mbele kutimiza masharti ya kujikinga na maambukizi ya Corona ikiwa ni kufuata masharti ya wataalamu wa afya.

Alisema ili wao wawe kioo katika jamii uomgozi huo umekuwa ukiwahimiza wafanyabiashara wote kuhakikisha wanavaa barakoa, kuwa na vitakasa mikono na kuvitumia muda wote, kunawa maji tiririka na sabuni kabla ya kupanda magari na baada ya kutelemuka katika magari ikiwa hawajaanza kuwahudumia wateja.

Alisema kuwa katika kusisitiza hilo uongozi na wafanyabiashara wote ambao wamekuwa na uelewa anapotokea mfanyabiashara mwenzao akakaidi kufanya hivyo hawamruhusu kupanda gari yoyote kwenda minadani kufanya biashara na badala yake ushushwa na kubaki.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya mipango na Fedha (UWABIMIDO), Gideon Mdumli alisema kuwa pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma kuwajali wafanyabiashara lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni kukosa eneo maalum ambalo umoja huo unaweza kujenga ofisi zao na kufanya shughuli zao.

Alisema kuwa walipo wamepanga hivyo wanahitaji kupata ardhi ili waweze kujenga ofisi zao zitakazoambatana na sehemu ya kuhifadhi bidhaa zao ambazo uzipeleka minadani kwa ajili ya kuziuza na kuwahudumia wananchi huko mnadani.

Jambo lingine amezishauri taasisi za kifedha kuona namna ya kuwekeza kwa wafanyabiashara hao waendao minadani kwani kwa sasa ni umoja ambao unatambulika kisheria na ni rahisi kuwekeza ili wafanyabiashara hao waweze kuwa na kipato imara sambamba na kuweza kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi ya serikali.

Kwa upande wake afisa Masoko wa Jiji la Dodoma James Yuna alisema yeye kama afisa masoko kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wameweza kuzungumza na wafanyabiashara hao na kuwaelewa tofauti na awali walivyokuwa wakifanya shughuli zao katika maeneo hatarishi na ambayo hayakuwa rasmi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!