July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara Jangwani wageukwa, wafukuzwa

Wamachinga wakigawana viwanja katika maeneo ya wazi ya Jangwani

Spread the love

MKUU wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi  amewapa siku tatu wafanyabiashara wadogowago eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam walio hamishwa kutoka kariakoo kubomoa vibanda walivyojenga kwa ajili ya bihashara na kudai kuwa ni wavamizi. Anaandika Hamisi Mguta na Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Wafanyabiashara hao waliokuwa wakifanya biashara kiholela kandokando ya barabara katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam baada ya kuwepo kwa mgogoro kati ya wafanyabiashara hao na manispaa ya Ilala.

Mushi amesema kuwa manispaa ya Ilala haijawahi kugawa eneo la jangwani kwa wafanya bihashara wa aina yeyote na eneo hilo si salama kwa makazi wala shughuli zozote za kiuchumi hali iliyopelekea kuwaita wafanya biashara hao kuwa ni wavamizi.

Aidha, ameongeza kuwa ifikapo julai 30 wafanyabiashara hao wanatakiwa wawe wameshavunja vibanda hivyo na atakaye kaidi agizo hilo atashitakiwa na kuvunjiwa kibanda chake.

Nae mfanyabiashara Oddo Kasunzu wa jangwani amesema Mkurugenzi wa manispaa hiyo alitangaza wafanyabiashara hao wahame kutoka kariakoo na kuwataka kuhamia jangwani takribani wiki mbili zilizopita, na waliagizwa kujenga vibanda vitakavyotumika kwa muda na sio kujenga kwa kutumia tofari, hali ilyowapelekea kujenga vibanda kwa kutumia mbao.

Mmoja wa wafanya biashara waliopo katika eneo hilo la jangwani Bi. Mariam Edward amesema kuwa serikali haiukuzingatia haki za wafanya biashara hao kwa kuwahamisha kariakoo na kuwahamishia jangwani ambapo bado kuna migogoro inayoendelea kati yao na serikali.

“Hatupo tayari kuhama katika eneo hilo kirahisi kwasababu tumetumia pesa nyingi kujenga vibanda na tutamshitaki mkurugenzi endapo atadiliki kubomoa vibanda vyetu.”amesema Mariam Edward

error: Content is protected !!