April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara Dodoma waonywa

Spread the love
WAFANYABISHARA¬† wa soko kuu la Majengo jijini hapa wameonywa kutowachagua viongozi wenye kuhamasisha migogoro ndani ya soko. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Pamoja na kuonywa kwa kutowachagua viongozi wa aina hiyo wameshauriwa kuwachagua viongozi wabunifu na wenye uwezo wa kuibua miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kutatua migogoro pale inapojitokeza.
Aidha viongozi watakaowachagua wawe pia na uwezo wa kielimu na uzoefu ambapo kwa pamoja sifa hizi zitawawezesha kuwa kiungo baina yao na wafanyabishara,watumishi wa halmashauri na kata.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Msinta Mayaoyao, alipokuwa akizungumza na wagombea wakati walipokuwa wakijinadi mbele ya wafanyabiashara wa soko hilo kwenye mkutano wao uliofanyika jijini hapa,
Alisema kuwa viongozi wanaohitajika kuongoza soko hilo ni wale wenye sifa za kimaendeleo na siyo wenye kufikiri jinsi ya kuhamasisha  migogoro isiyo kuwa na tija kwa ajili ya mfanyabishara.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya majengo alitaja adhara za kuwa na viongozi wasio na sifa wakichaguliwa wanaweza kurudisha nyuma maendeleo kwa wafanyabishara na hata kwa viongozi wenyewe.
Hata hivyo amewataka viongozi watakaochaguliwa kwa upande wao kuhakikisha wanaongoza ipasavyo kwa kufuata sheria kanuni katiba ya soko,ili waweze kutimiza malengo yao pamoja na kutoa ushirikiano kati na wafanyabiashara.
“Ninawaomba viongozi watakapata nafasi ya kuongoza hakikisheni mnaogoza kwa kufuata sheria na miongozo ya katiba yenu,na sivyo kwa kuangaliana sura,kabila,dini au rangi mkifanya hivyo soko hili linaweza kuingia kwenye hasara ya kukosa mapato yake ya serikali’alisema.
Katika uchaguzi huo viongozi wanaohitajika ni nafasi ya Mwenyekiti na msaidizi wake,Katibu na msaidizi,Mweka hazina pamoja na wajumbe watano wa kamati kuu ya soko hilo lililopo Majengo.
error: Content is protected !!