May 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyabiashara Dar waililia serikali Moro

Spread the love

SERIKALI imeombwa kuandaa vifungashio vinavyokwenda na mizani ili kuifanya sheria ya vipimo kutekelezeka, anaandika Christina Haule.

Lakini pia kufanya magari yanayobeba bidhaa zinazoharibika haraka (malimbichi) kupimwa kwa usahihi na haraka huku yakiondoka kwa wakati.

Wafanyabiashara wa viazi kutoka Buguruni, Temeke, Manzese, Mabibo na Mbagala jijini Dar es Salam wametoa ombi hilo leo wakiwa kwenye mizani ya Mikumi, Morogoro kufuatia magari yao kukamatwa tangu tarehe 7 Oktoba mwaka huu baada ya kudaiwa kujaza magunia ya bidhaa walizobeba zaidi ya kiwango (rumbesa).

Wafanyabiashara hao akiwemo Hussein Ally, dereva wa lori la mizigo hiyo wameeleza kukwazwa na hatua hiyo na kwamba, wamekaa hapo kwa zaidi ya siku tatu pasipo kujua kinachoendelea.

Pia wanaiomba Serikali ya Mkoa wa Morogoro kuwasaidia ili waendele na safari na kwamba, wameishiwa fedha za matumizi na si wenyeji katika maeneo hayo.

Ally amesema kuwa, wanalazimika kulalamikia sheria  hiyo ya vipimo kushindwa kutekelezeka kwa upande wao kutokana na serikali kutoandaa vifungashio pamoja na mizani kwa ajili ya kazi hiyo.

Hata hivyo amesema, hawaipingi sheria ya vipimo ila ni ngumu kutekelezeka kutokana na serikali kushidwa kuandaa mapema vifungashio sambamba na mizani kwa ajili ya kupimia huku mazingira ya shambani yakiwa magumu.

Baada ya kukamatwa kwa magari hayo, wafanyabiashara hao waliamua kwenda kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kujua uhalali wa kukamatwa.

Hata hivyo, Regina Chonjo, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambaye aliwaambia suala hilo liko kisheria na kuwa, hawawezi kuliingilia.

Wilson Kacholi, Meneja wa Vipimo kwa Mkoa wa Morogoro amesema, wamekuwa wakisimamia sheria hiyo kikamilifu sambamba na agizo la Waziri Mkuu la kutojaza rumbesa.

Na mwamba, vifungashio na mizani ni suala la wafanyabishara hivyo wanapaswa kuwa na vifaa hivyo  waendapo kununua mali zao.

 

error: Content is protected !!