Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wafahamu warithi wa tawala za wazazi wao
Habari Mchanganyiko

Wafahamu warithi wa tawala za wazazi wao

Ali Bongo Ondimba
Spread the love

 

MAHAMAT Idriss Déby Itno, ameapishwa kuwa rais mpya wa Jamhuri ya Chad. Amechukua nafasi ya baba yake, Idris Deby (68), aliyeuawa Jumanne iliyopita.

Kabla ya kufanywa kuwa rais, Déby (37), anayejulikana pia kama “Jenerali Kaka,” alikuwa msimamizi wa walinzi wa rais. Ataongoza nchi hiyo, kwa miezi 18 hadi kufanyika uchaguzi mkuu.

Mwaka 2009, alishiriki katika vita vya Am Dam, ambavyo vilipiganwa pia na binamu yake Timan Erdimi aliyemuita mjomba rais Idris Deby, mashariki mwa Chad.

Aliyekuwa Rais wa Chad-Idris Deby

Baba yake, Idris Deby, aliongoza Chad kwa miongo mitatu. Alishiriki mapambano kadhaa ya kijeshi wakati akihudumu kama rais. Huu ulikuwa muhula wake wa sita kuhudumu kwenye nafasi hiyo, katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Idris Deby alifikwa na mauti kufuatia shambulio la risasi lililofanywa na wanamgambo wanaopinga serikali yake, akiwa mstari wa mapambano.

Utawala wa kijeshi uvunja Bunge na serikali, ingawa wataalam wa katiba na sheria wanasema, Spika wa Bunge ndiye aliyepaswa kuongoza kipindi cha mpito, pale rais anapofariki dunia.

Joseph Kabisa

Kifo chake, kilitangazwa kwenye televisheni ya serikali, siku moja baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, ambayo yalionekana yangemrejesha mamlakani.

Hatua ya Jenerali Kaka, kurithi madaraka ya baba yake, limekuwa jambo la kawaida katika nchi kadhaa za Afrika; na au katika tawala za kifalme ulimwenguni.

Kwa mfano, ukimuondoa Mahamat Déby, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila Kabange, aliongoza taifa hilo, kufuatia kufariki kwa baba yake, Rais Laurent-Désiré Kabila.

Joseph Kabila, alianza kazi ya urais, siku 10 baada ya mauaji ya baba yake. Aliitawala Congo, kutoka Januari mwaka 2001 hadi Januari 2019.

Kabila mtoto alizaliwa tarehe 4 Juni 1971, katika mkoa wa Sud-Kivu, na alikuwa afisa wa jeshi na baadaye mwanasiasa.

El Hadj Omar Bongo Ondimba.

Mtoto huyo wa kiongozi wa waasi wa Congo – Laurent-Désiré Kabila – alikulia nchini Tanzania na alipata masomo yake nchini humo.

Alishiriki katika mapambano ya waasi waliomsaidia baba yake mwaka 1997, kumtoa Rais Mobutu Sese Seko.

Baada ya Laurent kuwa rais, Laurent-Désiré Kabila, alirudisha nchi kwa jina lake la asili – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutoka Zaire iliyoitwa na Mobutu Sese Seko.

Baada ya vita kumalizika, Joseph alipelekwa China kwa mafunzo zaidi ya kijeshi. Alipomaliza mafunzo yake na kurejea nyumbani, aliteuliwa mkuu wa jeshi na meja jenerali.

Naye Rais wa Togo, Faure Essozimna Gnassingbé Eyadéma, amerithi nafasi hiyo mwaka 2005, kutoka kwa baba yake, Gnassingbé Eyadéma.

Faure Essozimna, alizaliwa tarehe 6 Juni 1966 na amekuwa rais wa taifa hilo, tokea mwaka 2005.

Kabla ya kuwa rais, baba yake, alimfanya kuwa waziri kutoka mwaka 2003 hadi 2005.

Kufuatia kifo cha Rais Eyadéma, Gnassingbé akateuliwa haraka kuwa rais mpya kwa kutumia usaidizi wa jeshi.

Lakini mashaka juu ya ustahiki wake chini ya katiba ya nchi hiyo, yamempa shinikizo kubwa Gnassingbé.

Ali Bongo Ondimba

Alishinda pia uchaguzi wa rais uliokuwa na upinzani mkali wa tarehe 24 Aprili 2005, na akaapishwa kama rais. Alichaguliwa tena kuwa rais mwaka 2010.

Ali Bongo Ondimba, alichukua usukani wa nchi ya Gabon, Oktoba mwaka 2009, kufuatia kifo cha baba yake, El Hadj Omar Bongo Ondimba.

El Hadj Omar Bongo Ondimba, alikuwa rais wa pili wa nchi hiyo. Alitawala Gabon, kwa miaka 42 kutoka mwaka 1967 hadi mwaka 2009, alipofikwa na mauti.

Wakoasoaji wake wamemueleza kuwa rais huyo aliyeongoza taifa hilo tajiri kwa mafuta, alikuwa mfisidi aliyekubuhu. Yeye na mwanae wameiongoza Gabon kwa jumla ya miaka 54 sasa.

Mafuta yanachangia asilimia 60 ya uchumi wa nchi hiyo. Kwa sasa anaelekea kumaliza muhula wake wa miaka saba, lakini nchini Gabon, hakuna ukomo wa madaraka ya urais.

Katika Bara hili la Afrika, bado kuna nchi mbili ambazo zinaongozwa na wafalme – Morocco na Eswatini – ambazo ndio wenye mamlaka makuu ya utawala wa serikali.

Katika tawala hizo, ni jambo la kawaida na kikatiba kwa watoto wa wafalme kurithi madaraka wanapofariki ama kuondoka madarakani wazazi wao. Hawa ndio watawala wawili wa nchi hizo waliowarithi baba zao ufalme.

Mfalme MuhammEd Bin Sidi Alaouite wa Moroco alizaliwa mnamo 21 Agosti 1963, katika mji mkuu Rabat. Alichukua usukani wa uongozi, tarehe 23 Julai 1999, kufuatia kifo cha baba yake, Mfalme Hassan II.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Mfalme Mohammed wa Sita aliahidi kushughulikia umasikini na ufisadi kwa kuunda ajira na kuheshimu haki za binadamu.

Februari mwaka 2000, Mfalme Mohammed, alianzisha sheria mpya ya familia, ambayo inatoa uhamasishaji wa wanawake.

Mnamo Desemba 2020, Mfalme Mohammed VI alikubali kuimarisha uhusiano na Israeli chini ya makubaliano kuwa Marekani itatambua eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, kama lililo chini ya udhibiti wa Morocco.

Mfalme Mswati III (Makhosetive) alikuwa mtoto wa Mfalme Sobhuza wa Pili, aliyezaliwa na mmoja wa wake zake, Ntfombi Tfwala, 19 Aprili 1968 huko Manzini.

Alivishwa taji la Prince Mswati III, Ingwenyama, na baadaye akapewa taji la Mfalme wa Swaziland mnamo 25 Aprili 1986, akiwa na umri wa miaka 18, na kumfanya kuwa mfalme mchanga zaidi ulimwenguni wakati huo.

Mfalme Sobhuza II alikufa tarehe 21 Agosti 1982, ambapo Prince Makhosetive akafanywa mfalme mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!