October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadhamini wa Lissu ngoma mbichi

Robert Katula, mdhamini wa Tundu Lissu akitoka mahakamani

Spread the love

WADHAMINI wa Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, wamegomewa maombi yao kwamba ‘Lissu akamatwe’ waliyoyafikisha katika Mahakama Kuu ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Anaandika Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Upande wa mashtaka umetaka ombi la wadhamini wa Lissu lifutwe ambapo jana tarehe 14 Julai 2020,  Wakili wa Serikali Mkuu Simon  Wankyo,  mbele ya Hakimu Mkazi   Mkuu Thomas Simba aliitaka mahakama hiyo kutotoa hati ya kukamatwa kwa Lissu ambaye kwa miaka mitatu, amekuwa nje ya nchi kwa ajili matibabu ya majeraha ya risasi.

Lissu alishambuliwa kwa risasi 16, alipokuwa anawasili nyumbani kwake Area ‘D’ jijini Dodoma akitoka bungeni tarehe 7 Septemba 2017.

Ombi hilo lilifunguliwa na Robert Katula na Ibrahim Ahmed, waliomdhamini kwenye kesi namba 208 ya 2016 inayohusu tuhuma za uchochezi dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio pia mchapishaji wake.

Kesi hiyo inamuhusu Mhariri wa Mawio Simon Mkina, mwandishi mwandamizi Jabir Idrissa na mchapishaji wa Kampuni yaFlint, Ismail Mehboob.

Wankyo alieleza mahakama kwamba, dhamira ya kupinga ombi la wadhamini wa Lissu na kuwa, upande huo umepanga kuwalisilisha kwa maandishi na kuomba muda wa kuandaa hoja zao.

Wankyo amedai, mahakama hiyo tayari imeamua kuhusu ombi la kukamatwa kwa Lissu na kwamba  ililiondoa.

Hakimu Simba amesema, mawasilisho ya hoja za serikali yafanywe ifikapo tarehe 28 Julai 2020 na waombaji wajibu tarehe 11 Agosti na kutakuwa na haja ya kujibu upande ufanye hivyo tarehe 18 Agosti 2020. Usikilizaji utafanyika tarehe 19 Agosti mwaka huu.

Kwenye kesi ya msingi, watuhumiwa wanashtakiwa kwa mashtakamatatu ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio kwa kuchapisha habari yenye kichwa ‘Machafuko yaja Z’bar.’ Watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana ,

Kukosekana kwa Lissu kesi hiyo inapotajwa kumechangia mahakaa kuwabana wadhamini wamfikishe mahakamani mtuhumiwa kwa kuwa ndio jukumu lao kisheria.

 

error: Content is protected !!