Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wataka TEHAMA isiwaache nyuma wenye ulemavu
Habari Mchanganyiko

Wadau wataka TEHAMA isiwaache nyuma wenye ulemavu

Spread the love

WADAU wa masuala ya haki za binadamu Tanzania, wameiomba Serikali iweke mikakati itakayohakikisha matumizi ya Teknokojia ya Habari na Mawasiliano, haiwaachi nyuma watu wenye ulemavu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa jana tarehe 8 Machi 2023 katika  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema ni wajibu wa Serikali kuhakikusha ubunifu na mabadiliko ya teknolojia, yanakuwa Chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.

“Tunapaswa kuangalia je, uwepo wa teknolojia ya habari na mawasiliano na masuala ya mtandao imekuja kuongeza chachu ya ninyi watu wenye ulemavu kufanya kazi au imekuja kuwatenga na jamii nyingine. Je, mazingira ya sheria, sera na mifumo yetu inazingatia Kuna watetezi wa haki za binadamu ulemavu,” amesema Olengurumwa.

Mtetezi huyo wa haki za binadamu ametahadharisha kuwa, kama mitandao haitasimamiwa kwa umakini inaweza leta utengabo au ubaguzi mkubwa kati ya jamii Moja na nyingine.

“Yale makundi ambayo yana uwezo wa haraka kufikia teknolojia hii wakayaacha makundi ya watu wenye uhitaji maalum, kwa sababu ya mazingira na kwa sababu za kiuchumi,” amesema Olengurumwa.

Naye Mkurugezi wa Tanzania Epilepsy Foundation, Fides Uiso ameomba wadau mbalimbali ikiwemo THRDC, kuendelea kuwaamini na kuwawezesha kwa kuwajengea uwezo wa kidigitali watetezi wa haki za watu wenye uhitaji maalumu, ili waendelee kupata ujuzi zaidi wa kutetea makundi hayo.

Mkurugezi huyo kutoka Shirika linalowahudumia watu wenye Kifafa,   amesema makundi hayo bado yana changamoto ya utumiaji wa mifumo ya kidigitali hali ambayo inapelekea ugumu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkurugezi wa Shirika la Sauti ya Wanawake wenye ulemavu Tanzania ( SWAUTA), Stella Jailos, ameshauri Serikali kuundwa kikosi kazi cha kuangalia kama mifumo ya kidigitali iliyopo kwa sasa inanufaisha Watetezi wa watu wenye uhitaji maalumu.

“Kitengenezwe kikosi kazi kutoka kwa wanawake wenye ulemavu ili kuweza kupembua sera za Nchi hii kuona mwanamke mwenye ulemavu amewekwa vipi na kama hajawekwa kwenye sera washauri nini kifanyike kwa kutoa mapendekezo kwa Serikali,” amesema Jailos.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!