December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wadau wasusia kikao cha kanuni za usalama

Inspekta, Deus Sokoni akiwasilisha sheria mpya za Usalama barabarani zitakazoanza kutumika kesho nchi nzima

Inspekta, Deus Sokoni akiwasilisha sheria mpya za Usalama barabarani zitakazoanza kutumika kesho nchi nzima

Spread the love

UMOJA wa wasafirishaji mizigo (TATOA) na umoja wa madereva wa mabasi Tanzania (UWAMATA), wamesusia kikao cha Baraza la Taifa la usalama barabarani, baada ya kutofautiana wakati wa uwasilishwaji wa kanuni mpya za usalama barabarani. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Sintofahamu hiyo imetokea katikati ya kikao hicho kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee Dar es salaam, ambapo wadau hao walinyimwa nafasi ya kuchangia hoja zao, na kulazimishwa kufuata kanuni zilizopangwa.

Akizungumza katibu mkuu wa Uwamata, Abdallah Lubala amesema, waliamua kuondoka ndani ya kikao hicho kwa kuwa hawathaminiwi, hawakushirikishwa katika upitishwaji wa kanuni hizo, na kwamba kuna mapendekezo ambayo waliyatoa lakini hayajatendewa kazi.

“Mimi naona wanatupotezea muda tu kwa sababu  tulijua leo tunakuja kujadili na kuwasilisha changamoto zetu ili ziwekwe kwenye kanuni kumbe si hivyo, wao wameshapendekeza za kwao na wameshazipitisha sasa wametuita ili iweje? Hawajatenda haki sheria zote zinatubana sisi.” Amesema Lubala.

Naye  afisa mnazimu wa kikosi cha usalama barabarani, Johansen Kahatono amefafanua kuwa, mnamo tarehe 4, Novemba mwaka  jana walikaa kikao na wadau mbalimbali wa usafirishaji na kukajadili kwa pamoja kanuni hizo na zikapitishwa.

Aidha, Kahatono amebainisha kanuni hizo mpya kuwa ni, elimu kwa madereva, upimaji afya, kufunga camera kwenye magari ya kuruhusu magari na kubandika alama zinazoonekana kwenye magari ya kubeba mizigo.

Amesema, kanuni hizo wameziweka ili kukomesha ajali za makusudi barabarani na kunusuru maisha ya watanzania kwa ujumla, pia kulipa urahisi jeshi la polisi kuwakamata wahalifu na sio kuwabana madereva wala wamiliki wa mabasi.

Ameeleza kuwa dereva yoyote atakayevunja sheria barabarani atachukuliwa hatua za kisheria. Makosa kama, lugha mbaya, ulevi, kunyanyasa abiria, madereva hao watapigwa faini au kurudishwa tena shule ya udereva au kufungiwa leseni yake.

Ameongeza kuwa mabsi ya abiria, mizigo watatakiwa kurudi shule kila baada ya miaka mitatu ili kupata leseni mpya, na wamiliki wa magari binafsi watatakiwa kurudi shule baada ya miaka sita.

error: Content is protected !!