Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Wadau wasisitiza kutunza amani Kenya
Makala & Uchambuzi

Wadau wasisitiza kutunza amani Kenya

Vurugu za mauaji ya Kenya yaliyowahi kutoka mwaka 2007
Spread the love

WITO wa amani umeendelea kutolewa kwa wananchi nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu, ili kuepusha machafuko yaliyozuka katika uchaguzi wa mwaka 2007, anaandika Catherine Kayombo.

Miongoni mwa waliotoa wito huo ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, Wafula Chebukati kufuatia kifo cha aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa masuala ya teknolijia katika tume hiyo, Christopher Musando.

Wafula amewataka Wakenya kuwa wavumilivu na kulinda amani, na kutoruhusu hasira na chuki kuwatawala.

“Tusipo angalia, tutaiweka nchi yetu matatani. Kama tume, tunaahidi kusimamia uchaguzi, kuondoka kwa musando kumerudisha hatua tulizopiga lakini haimaanishi hatutofanya kazi yetu”, aliwaambia wanahabari.

Wakati huo huo, muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA umeitaka tume ya uchaguzi kumuajiri mtaalamu mpya wa kimataifa kutoka nje nchi ili kushughulikia idara ya teknolojia.

Haya yanajiri wakati mamia ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu waliandamana jana, Agosti mosi jijini Nairobi kulaani mauaji ya meneja huyo wa teknolojia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wamesahau aliyofanya Magufuli

Spread the loveJUMATATU ya tarehe 16 Oktoba 2023 itabaki kuwa siku ya...

error: Content is protected !!