March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wadau washauri kufufuliwa chuo cha Tetemeko

Spread the love

SERIKALI  imetakiwa kufufua chuo cha elimu ya tetemeko la ardhi kilichowepo mkoani Dodoma ili kuwafanya Watanzania kutambua na kujikinga mapema na madhara ya tetemeko, anaandika Christina Haule.

Ombi hilo lilitolewa na Makamu wa Rais wa Chama cha Wasanifu Majengo Tanzania (AAT),  Tchawi Mike.

Ameyasema hayo alipofungua mafunzo ya kuwajenea uwezo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari na asasi zisizokuwa za serikali ambayo yaliandaliwa na  Mpango wa Uwazi katika Sekta ya Ujenzi Tanzania (CoST).

Tchawi amesema Tanzana ni kati ya inayopitiwa na Mabonde ya ufa mawili la mashariki na magharibi ambayo yanatoa matetemeko yanapofukutika na wakati mwingine kwa kasi kubwa yenye ukubwa wa richa skeli 8  kila baada ya miaka 50.

Amesema elimu ya tetetemeko la ardhi inapaswa kurejeshwa kama ilivyokuwa ikitolewa zamani katika chuo kilichokuwa mkoani Dodoma ili kuwafanya Watanzania wengi  kupata  uelewa.

Ameongeza kuwa tetemeko ya ardhi ni janga linalotokea katika nchi mbalmbali bila watu kujua na kuleta athari mbalimbali ikiwemo za vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Tetemeko lililowahi kutokea mkoani Bukoba lilikuwa la richa skeli 5.2 ambapo licha ya kuleta madhara makubwa, ingawa zile zilizojengwa  kwa kwa udongo na miti au fito hazikuathirika.

“Wazee wa zamani walijenga nyumba za matope,  lakini walikuwa wakifunga fito kama ringi na kusababisha wakati wa tetemeko nyumba kutoanguka” amefafanua  Tchawi.

Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa maeneo yanayoguswa Tetemeko kila wakati  na kwamba kuna haja ya kujengwa majengo ambayo tahadhari zote zinachukuliwa.

Tetemeko kubwa la richa skeli 8 linaweza kutokea katika mkoa wa Mpanda nchini Tanzania kufuatia mkoa huo kuwa na hatari ya mabonde yote mawili kukutana katika njia moja

error: Content is protected !!