Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Wadau waombwa kusaidia taulo za kike kwa watoto yatima
Habari Mchanganyiko

Wadau waombwa kusaidia taulo za kike kwa watoto yatima

Mjasiliamali Saida Msuya akionesha moja ya boksi la taulo za kike (pedi) alizopeleka kwenye kituo cha vijana wenye ulemavu wa akili cha MEHAYO
Spread the love

SERIKALI na wadau mbalimbali wameombwa kutoa msaada taulo za kike (pedi) kwa mabinti waliopo kwenye vituo vya kulelea watoto yatima na walemavu kufuatia watoto hao kutokuwa na uhakika wa kuzipata. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mkurugenzi mwanzilishi wa kituo cha vijana wenye ulemavu wa akili (MEHAYO), Linda Ngido alisema hayo jana wakati akipokea msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho ikiwemo pedi za watoto wa kike vilivyotolewa na Mjasiliamali Saida Msuya maarufu kama Mama Halima Fashion wa mjini Morogoro.

Alisema, wamekuwa wakipata taulo za kike kwa ajili ya walemavu hao kutoka kwa watu mbalimbali na kwamba hawana uhakika wa kupata taulo hizo jambo ambalo limekuwa ni changamoto kwao katika kuwahudumia na kulazimika kuwavalisha sketi nyeusi.

Alisema, kituo hicho kwa sasa kina watoto 68 wanawake wakiwa 34 na wanaume 34 wengi wao wakitokea vituo vya kulelea watoto yatima na majumbani mwao.

Ngido alisema, lengo la kujiajiri wenyewe watoto hao limeonekana kuwa haliwezekani kutokana na akili zao na kwamba wakaomba eneo jingine kubwa katika eneo la Mkundi na kuandaa kwa ajili yao ili waweze kujimudu na maisha yao hata hapo baadae ikiwemo shughuli hizo walizojifunza kuzifanya wakiwa hapo kama nyumbani kwao.

Hata hivyo aliwaasa wazazi wanapopata watoto wenye ulemavu wa akili kujenga tabia ya kuwasaidia wakiwa na umri mdogo badala ya kuwafungia ndani huku wakiwaona hawawezi kufanya chochote hadi wanapofikia wakubwa na kuwapeleka MEHAYO jambo ambalo linamrudisa nyuma maendeleo ya mtoto.

“Wapo watoto wenye ulemavu wa viungo na akili ambao hufika hapa wakiwa hawajui lolote huku wakizidiwa na ulemavu lakini kama wazazi wao wangewapeleka kwenye vitengo vya mazoezi mapema wangeweza kupata nafuu japo kidogo” Alisema.

Pia aliwataka wazazi kuwa na maneno mazuri kwa watoto hao kwani suala la wazazi kuwa na maneno makali kwa watoto wao mara wanapogundua ulemavu wao linawafanya watoto hao kukosa amani ya moyo na kujikuta wakijitenga zaidi na kuona hakuna haja ya kukaa nyumbani.

Naye Mjasiriamali Saida Msuya alisema, alipata wazo la kutoa msaada kwa wahitaji baada ya kupata tuzo ya mjasiliamali bora mdogo (City bank) na kupata kiasi cha dola 6,000 ambazo ni sawa na Sh. 14 milioni baada ya kushinda tuzo ya ujasiliamali bora na kununua vifaa kwa ajili ya watoto hao.

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!