Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau waiangukia Serikali ajira za utotoni, wasichana kuachwa nyuma kidigitali
Habari Mchanganyiko

Wadau waiangukia Serikali ajira za utotoni, wasichana kuachwa nyuma kidigitali

Julieth Sewava, mwanzilishi wa program ya mtandaoni ya kutambua dawa bandia (Ephama Mobile Application)
Spread the love

 

ASASI za Kiraia nchini Tanzania, zimeiomba Serikali itafute muarobaini wa changamoto ya ajira za utotoni na wasichana kuachwa nyuma katika fursa zinazotokana na Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Anaripoti Regina Mkonde, Dares Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 5 Oktoba 2021, katika uzinduzi wa wiki ya uhamasishaji ushirikishwaji mtoto wa kike katika mapinduzi ya kidigitali, inayotarajiwa kufanyika mkoani Pwani na Dar es Salaam, itakatofikia kilele tarehe 11 Oktoba mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanywa na Muungano wa asasi za kiraia 40, za kupinga ajira za utotoni nchini Tanzania (TCACL) na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), huku mgeni rasmi alikuwa mhitimu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Tambaza, jijini Dar es Salaam, Julieth Sewava.

Sewava ameiomba Serikali kuweka mazingira rafiki ili kuwezesha watoto wa kike, wasiachwe nyuma katika masuala ya teknolojia na kidigitali.

Sewava ambaye ni mwanzilishi wa program ya mtandaoni ya kutambua dawa bandia (Ephama Mobile Application), amesema “uwakilishi wa wanawake katika teknolojia sio mada mpya, ingawa kuna maboresho lakini ni ya polepole sana, hivyo inahitajika nguvu zaidi.”

Sewava amesema, Serikali na jamii inatakiwa kuvunja nadharia ya kwamba watoto wa kike hawawezi kufanya vizuri katika masuala ya sayansi na teknolojia.

Mratibu wa TCACL, Scholastica Pembe

“Nitoe rai kwa Serikali na mashirika binafsi na wadau wote wa maendeleo ya mtoto wa kike kushirikiana pamoja katika kuhakikisha kila mtoto wa kike anapata fursa ya kunufaika na mazuri mengi ya ambayo teknolojia inaleta hasa kjatika karne hii,” amesema Sewava na kuongeza:

“Serikali na wadau ina jukumu kubwa la kuhakikisha watu wneye ulemavu wanapewa kipaumbele katika masuala ya kidigitali ili wasiachwe nyuma kundi hili mara nyingine limekwua likisahauliwa katika amsuala mbalimbaliu hivyo naow asiachwe.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mratibu wa TCACL, Scholastica Pembe, amesema jamii inakabiliwa na changamoto ya ajira za utotoni hasa katika shughuli za mashambani, migodini na mitaani.

“Ajira kwa watoto ina athari kubwa sana, na kwa sasa kuna zaidi ya watoto milioni 150 wanaendelea kupata shida kuhusiana na ajira kwa watoto, ikiwemo Tanzania. Changamoto kubwa ipo katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo utakuta watoto wengi wanafanya ajira za watoto hasa wanaoishi mitaani,” amesema Pembe.

Pembe amesema “ maeneo mengine ambayo kuna changamoto hiyo, ni maeneo ya kilimo, kumekuwa na tatizo la watoto kufanyishwa kazi hasa kwenye amshamba ya tumbaku na kahawa.”

Mratibu wa maadhimisho ya wiki ya mtoto wa kike, Radhia Mallah

Kufuatia changamoto hiyo, Pembe ameiomba Serikali na wadau mbalimbali kutafuta suluhu ya changamoto hiyo.

“Ninachoshauri kifanyike ili kukomesha changamoto hiyo, ni kutoa elimu katika ngazi ya familia, sababu ajira kwa watoto zinaanzia katika ngazi ya kifamilia. Tunashauri wadau na Serikali kutatua changamoto hiyo,” amesema Pembe.

Akizungumzia uzinduzi wa wiki hiyo, itakayo hitimishwa tarehe 11 Oktoba 2021 katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani, Mratibu wa maadhimisho hayo, Radhia Mallah, amesema watatumia fursa hiyo kutoa hamasa kwa jamii juu ya namna ya kuwainua watoto wa kike.

Amesema maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kwenye wilaya za Chalinze, Mkuranga na Kibiti mkoani Pwani na Ilala mkoani Dar es Salaam.

“Kupitia kauli mbiu ya kitaifa ‘Kizazi Cha Kidijitali, Kizazi Chetu” tunaungana na Serikali kuikumbusha jamii kutoa haki sawa kwa watoto wote kwenye teknolojia ya kidijitali ili waweze kuitumia kwa Maendeleo na Ustawi wao,” amesema Mallah.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!