Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa sekta binafsi wakutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Habari Mchanganyiko

Wadau wa sekta binafsi wakutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameshiriki katika ufunguzi wa kongamano kati ya Sekta ya Uchukuzi na wadau wa sekta Binafsi (Ministerial Public Private Sector Dialogue – MPPD) lililofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Aprili 11, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Kongamano limekusudiwa kujadili shughuli zilizofanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika sekta ya uchukuzi, changamoto zinazoikumba sekta ya uchukuzi, mafanikio ndani ya mwaka mzima, pia kujadili sera na mikakati ya nchi inayolenga kukuza sekta ya uchukuzi nchini ili kuleta mafanikio.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezitaka Mamlaka za Serikali kushirikiana na wafanya biashara kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa haraka ili kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara Tanzania.

“Nipende kusema kuwa sekta binafsi ni wadau wakubwa sana wa Serikali, pengine kuna kanuni au taratibu ambazo zinawakwaza, sisi tuko maofisini nyinyi mnafahamu kuliko sisi, kupitia mikutano hii tunaamini tunaweza kujua na kuzifanyia kazi,” amesema Mbarawa.

Aidha, Mbarawa ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) imelenga kujadiliana na sekta binafsi kupitia mikutano na makongamano mbalimbali ili kuzifahamu fursa, maboresho ya Sera, Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kujenga mzingira mazuri ya biashara.

“Ndugu washiriki Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuagiza kwamba Wizara ikutane na sekta binafsi katika maeneo yetu ili kupokea maoni, changamoto na maboresho ya sera, Sheria na miongozo mbalimbali kwasababu bila kuwa na Sheria nzuri na kanuni nzuri zinazoendana na wakati hatuwezi kufanya biashara na kushindana na wengine,” amesema Mbarawa.

Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini Angelina Ngalula amesema sekta ya uchukuzi inasaidia katika kupunguza gharama za bidhaa zinazozalishwa hapa nchini haswa katika sekta ya kilimo hivyo kuitaka Serikali iipe sekta ya uchukuzi kipaumbele kwa kuendeleza miundombinu ikiwemo reli na barabara.

“Ukuaji wa sekta ya uchukuzi, itasaidia katika kupunguza gharama za bidhaa zinazozalishwa nchini hasa za kilimo, utakuta bidhaa kutoka China inauzwa gharama kuliko inayozalishwa hapa nchini, hii ni kutokana na gharama kubwa katika usafirishaji,” amesema Ngalula.

“Nchi yetu ni ya kimkakati na ina fursa nyingi sana, katika sekta hii tutambue sisi ni wanachama wa SADC, kwa hiyo tunapojadili Sera, mikakati na mambo madhubuti ya nchi, lazima tutunge Sera zinazoendana na ushindani wa soko, zikiwa ni Sera tofauti sisi ndio tutakaopoteza zaidi,” alisema Angelina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!