Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wadau wa kilimo hai Tanzania waungana na Serikali
Habari Mchanganyiko

Wadau wa kilimo hai Tanzania waungana na Serikali

Shamba la mpunga
Shamba la mpunga
Spread the love

 

UAMUZI wa Wizara ya Kilimo Tanzania Bara na Zanzibar, kutangaza kuwa zitatenga bajeti, kuanzisha kitengo na benki ya mbegu asili umepokelewa kwa mtazamo chanya na wadau wa Kilimo Hai Tanzania. Anaripoti Selemani Msuya, Dodoma

Wakizungumza na kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki jijini Dodoma, baadhi ya wadau wa kilimo hai wamesema kwa miaka mingi ya kupigania uwekezaji katika eneo hilo hakukuwa na utashi wa Serikali kama ambao umetangwaza na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Mashiriki yasiyo ya Kiserikali yanayohamasisha utunzaji wa Baionoai ya Kilimo Tanzania (TABIO), Abdallah Ramadhan alisema kwa muda mrefu walikuwa watamani kuona mikakati kama ambayo Serikali imeaniasha ili kusukuma gurudumu hili la kilimo hai.

Alisema kilimo hai kimekuwa kikizungumzwa bila kuwepo kwenye sheria, sera na mikakati hivyo ujio wa kitengo utafungua kurasa mpya katika sekta ya kilimo hasa kilimo hai.

“Haya ambayo yameanishwa na Serikali zote mbili kuwa zitatenga bajeti, kuanzisha benki ya mbegu asili na kuunda vitengo yanaweza kuwa na tija kama wadau wote watashiriki kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa,” alisema.

Alisema kilimo hai ni uhai sahihi kwa maisha ya viumbe vyote hasa binadamu kwa kuwa inachangia kupata chakula bora na salama.

Ramadhan alisema kwa taarifa za sasa zinadhibitisha kuwa duniani afya za watu zimetetereka hivyo nguvu kubwa inatakiwa kuelekezwa kwenye kilimo hai.
Mtaribu huyo alisema matumizi ya dawa zenye kemikali nyingi kwenye kilimo zinachangia kuharibu mazingira na ardhi kushindwa kuwa endelevu.

Alisema TABIO imeajipanga vizuri kuhakikisha kilimo hai kinafikia kila mtu ambaye anajihusisha na kilimo ila hilo litafanikiwa iwapo Serikali kupitia taasisi zake za kilimo zinashiriki.

Kwa upande wake Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Afrika (AfrONet), Constantine Akitanda alisema kilichofanywa na Serikali juzi ni kupiga hatua moja mbele hali ambayo inaungwa mkono na shirika lao.

Alisema AfrONet inahamasisha kilimo hai kupitia ofisi za Kilimo Hai katika nchi husika hivyo ni imani yao kuwa kauli ya Serikali itachochea mabadiliko kwenye sekta ya kilimo.

Akitanda alisema bodi ya wakurugenzi ya AfrONet imeunga mkono juhudi hizo ambazo wanaamini zitaweza kukuza uchumi wa wakulima na nchi kwa ujumla.
“Sisi tutasaidia kujenga uwezo na kuhamasisha sera ziwepo katika nchi za Afrika ili kuhakikisha Mpango wa wa Maendeleo wa Afrika wa 2063 na Maendeleo Endelevu (SDGs) ifanikiwa kwa pamoja.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Dk. Mwatima Juma alisema kilimo hai nchini kitapata mafanikio iwapo utafiti na utashi wa kisiasa vitaenda pamoja.

Dk. Juma alisema kilimo hai ndio kitawezesha afya, mazingira na mabadiliko ya tabianchi kuwa salama na endelevu hivyo kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi.
“Kilimo Hai kinachangia usalama wa chakula, masoko, kuvutia watalii na kuchochea ukuaji wa uchumi,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!