December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadau: Vyombo vya habari ni mlezi wa demokrasia

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer

Spread the love

 

VYOMBO vya habari nchini Tanzania, vimetajwa kuwa mlezi wa demokrasia na utawala Bora, endapo vitatekeleza majukumu yake kikamilifu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa Leo Alhamisi, tarehe 20 Oktoba 2022, jijini Dar es Salaam, katika mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Kwa ajili ya kujadili sheria za habari nchini.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer, amesema uhuru wa vyombo vya habari unachagiza maendeleo ya demokrasia na sera nzuri.

Amesema Ubalozi wa Uholanzi uko tayari kuendelea kushirikiana na TEF katika kuimarisha tasnia ya habari nchini, kupitia njia mbalimbali ikiwemo kufadhili harakati za uchechemuzi wa mabadiliko ya Sheria zinazosimamia vyombo vya habari.

Kwa Sasa, Ubalozi wa Uholanzi unafadhili shughuli za uchechemuzi wa marekebisho ya Sheria za habari zinazosimamiwa na TEF.

Naye Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema vyombo vya habari vinasaidia wananchi kupata uelewa mkubwa kuhusu haki zao na wajibu wao katika kuleta maendeleo.

“Wananchi wanapokuwa na uelewa mkubwa katika jamii, demokrasia itakuwa sababu watafanya uamuzi sahihi, wanamtaka Fulani SI Kwa sababu amepewa kanga wakati wa kampeni lakini ameahidiwa kukuza elimi, miundombinu na uchumi,” amesema Balile.

error: Content is protected !!