January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadau: UDA-RT Wizi mtupu

Spread the love

MPANGO wa Uda Rapit Transit (UDA-RT) umepingwa. Wadau wa usafirishaji waukosoa, wasema ni wizi mtupu na kutaka upitiwe upya. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mpango huo umepigwa leo katika ukumbi wa Karemjee Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoshirikisha wadau hao ili kukusanya maoni ya kiwango cha nauli zitakazotumika kwenye usafiri wa mabasi ya mwendo kasi unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Awali UDA-RT walipeleka mapendekezo yao kuhusu kiwango cha nauli ziitakazotumika kwenye usafiri huo Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu mtendaji Baraza la Ushari wa Watumiaji wa Usafiri wan chi kavu na majini (Sumatra) Oscar Kikoyo amesema walijiridhisha kuwa maombi yaliyowasilishwa  hayana weledi.

Kikoyo amesema, katika maelezo yaliyopelekwa na UDA- RT hayakutimiza viwango vinavyotakiwa na kwamba, mambo mengi hayakuwekwa bayana kama ilivyo tarajiwa.

Ameeleza baadhi ya mapendekezo yaliyopelekwa na UDA –RT ni pamoja na nauli kuwa katika njia kuu ya Kimara kwenda Kivukoni itakuwa sh. 1,200, njia ya mlisho na njia kuu itakuwa sh. 1400 na nauli ya njia ya mlisho Mbezi Kimara itakuwa sh.700

Mapendekezo yaliyotolewa na UDA-RT kwa kupitia Mkurugenzi mtendaji wa mradi huo David Mgwassa yameonekana kutokuwa wazi na hayawanufaisha wananchi.

Hivyo, Kikoyo amependekeza kuwa yapitiwe upya, kwani baada ya kupitia na kufanya ukokotozi wamebaini kuwa hakukuwa na haja ya kupandisha nauli wala kuyazuia mabasi mengine kutofanya kazi.

Aidha ameeleza kuwa, licha ya mapendekezo hayo kuwa na kasoro nyingi lakini bado yana mapungufu makubwa ikiwemo ya kutopeleka kibali cha kufanya mradi huo hapa nchini, pia wamependekeza kuwa nauli iendelee kutumika hii iliyopo.

Pia ameitaka UDA-RT iweke  wazi mikataba yao na Serikali na mikataba yao na waajiri wao. “tunataka kujua kwamba mkataba ni wa muda gani? Isije kuwa mmesaini mkataba wa miaka 50 tukashidwa kufika au mmesaini mkataba wa mwaka mmoja tusije kuwa tunapoteza muda tu”

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Chama Cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) Hassani Mchanjama amependekeza kuwa  endapo Serikali ikiuruhusu mpango huu basi iwe tayari kuruhusu wamiliki wa daladala nao wapandishe nauli.

“DAT- RT haikufanya utafiti kabla ya kutaka kuanzisha huo mradi. hawapo kwaajili ya kuwasaida wananchi bali wapo kwa manufaa yao kwani hakuna haja ya kupandisha bei wakati kila siku mafuta yanapungua bei” amesema Mchanjama.

Kwa upade wake Mkurugenzi wa Sumatra  Gilliard Ngewe amewataka wadau kuendelea kutoa maoni ndani ya siku 14 tangu kupelekwa kwa mapendekezo ya UDA-RT  kisha yatajadiliwa na kutolewa uamuzi baada ya kupatikana muafaka.

“Leo hapa tupo kwaajili ya kukusanya maoni tu na sio kutoa kiwango ch nauli wala kutoa hukumu yoyote. Tutayarekodi mawazo yote yatakayotolewa kisha tutawataarifu kilichokubaliwa,” amesema Ngewe.

error: Content is protected !!