January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadau: Ratiba ya NEC inaibeba CCM

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Jaji Damian Lubuva wakati akiapishwa na Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa ratiba ya uteuzi wa wagombea urais, ubunge na madiwani, kampeni na siku ya kupiga kura huku ikiacha mashaka makubwa. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).

Hata hivyo, ratiba hiyo imeibua maswali mazito kwa wadau, wakihoji inakuwaje NEC inafanya hivyo siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza ratiba ya mchakato wake.

CCM imetangaza ratiba yake jana kuhusu utaraibu wa uchukuaji fomu kwa wagombea udiwani, ubunge na urais kuanzia Juni 3 na kurejesha kabla ya Julai 2 saa 10:00 jioni.

Wanaohoji ratiba hiyo, wanajenga hoja kwamba, NEC ilisubiri kwanza CCM itoe utaratibu wake ndio maana ratiba hiyo ikasainiwa 23 Mei 2015, siku ya Jumamosi ambayo sio ya kazi kiserikali lakini ikatolewa kwa Umma 25 Mei 2015.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, “Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuviarifu vyama vya siasa na wananchi wote kwa ujumla kuwa kwa mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35 B (1), (3) (a), 37 (1)(a) na 46 (1) vya Sheria ya NEC, Sura ya 343, ratiba ya uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo.”

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema kuwa, 21 Agosti, 2015, itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea urais, ubunge na udiwani.

Tarehe 22 Agosti hadi 24, 2015, utakuwa muda wa kuanza na kufunga kampeni, huku Oktoba 25, itakuwa siku ya uchaguzi mkuu.

Mmoja wa wadau wanaopinga utendaji wa NEC, ameliambia MwanaHALISIOnline “Nimeona ratiba ya NEC. Walikuwa wanasubiri ratiba ya CCM. Ni aibu tumekupanga ratiba kwa kufuata matakwa ya vyama badala ya tume kutoa ratiba ya kuviongoza vyama.

“Kwanza, ratiba haijakamilika. Matokeo yatatangazwa lini? Kama hakuna ‘limit’ ya kutangaza matokeo maana yake tunapiga kura ambazo hatujui matokeo yake lini. Wanataka wapate muda wa kuchakachua?

error: Content is protected !!