Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wadau kupeana uzoefu ubunifu wa kiteknolojia
Elimu

Wadau kupeana uzoefu ubunifu wa kiteknolojia

Meneja wa Ubunifu wa Costech, Dk. Athman Mgumia
Spread the love

 

WADAU wa ubunifu wa teknolojia katika masuala ya kilimo, fedha na elimu wamekutana jijini Dar es Salaam kubadilishana uzoefu ili kukuza bunifu zao.

Mpango huo unaratibiwa na Kitengo cha ubunifu cha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Akizungumza na waandishi habari leo Novemba 3, 2022  jijini Dar es Salaam, Meneja wa Ubunifu wa Costech, Dk. Athman Mgumia amesema wadau hao wamekutana kubadilishana uzoefu na kutengeneza mahusiano yatakayowawezesha kuendeleza bunifu zao za kiteknolojia.

Dk. Mgumia amesema mpango huo ni wa ushirikiano baina ya nchi za Bara la Afrika na zile za Bara la Ulaya.

Amesema mpango huo ni jukwaa la fursa kwa wajasiriamali kupanua mbawa zao hasa kwenye eneo la ubunifu wa kiteknolojia.

“Jukwaa hili lipo kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kushirikiana katika fursa kwa wajaasiriamali na wadau Teknolojia ya Kidigitali waliopo nchini Tanzania na wenzao waliopo katika nchi nyingine Afrika na kule barani Ulaya,” amesema.

Amesema wabunifu hao wanaweza kushirikiana katika kuendeleza ubunifu katika maeneo ya teknolojia ya kilimo (Agritech), miamala ya fedha (fintech) na elimu.

Ametaja lengo lingine ni kutoa fursa kwa wajasiriamali na wabunifu kuanzisha mahusiano ya kimkakati katika kuendeleza bunifu zao za kijaasiriamali walizozianzisha kwa kupata uzoefu kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika na nchi za Ulaya.

Amesema kuwa jukwaa hilo linaendeshwa sambamba na majukwa mengine yanayoendesha kwenye nchi nyingine kama lile la Uganda, Ghana na Nigeria kwa Afrika  na Italia kwa upande wa Ulaya.

Amesema pamoja na kupata mawasilisho ya wataalamu katika masuala mbalimbali lakini wadau wanapata fursa ya kuhusiana wao kwa wao.

Rose Funja mmoja wa washiriki wa warsha hiyo ambaye ni mbunifu wa teknolojia ya drone (ndege nyuki) kwenye kukusanya takwimu za kilimo na Mawasiliano, amesema kuwa wanatumia teknolojia hiyo kukusanya picha na taarifa mbalimbali kupitia mionzi ambayo inaonekana kwa macho na ile isiyooneka kwa macho ambapo kwenye kilimo wanaitumia kujua mimea ina afya kiasi gani.

“Tunaitumia teknolojia hiyo katika kuwashauri wakulima kwa sababu inaonyesha mimea ipi imeharibika,” amesema Funja.

Amesema tayari washafanya mradi wa Kilimanjaro Agriculture Devolpment kwenye shamba la Mpunga ambapo walitumia drone na kukusanya taarifa na kuwashauri wakulima juu ya matokeo ya data hizo.

Justine Mwakatobe mkuu wa Idara ya Ubinifu na Atamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya (Must), amesema amejifunza namna ya kutumia teknolojia kwenye upande wa elimu na kilimo.

“Ujuzi nilioupata hapa nitakwenda kuwasaidia wabunifu waliokuwa chuoni kwetu kwa sababu chuoni kwetu tunawabunifu,” amesema Mwakatobe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!