Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Wadau kumchukulia Karia fomu Urais TFF
MichezoTangulizi

Wadau kumchukulia Karia fomu Urais TFF

Walace Karia, Rais wa TFF
Spread the love

 

BAADA ya kufunguliwa kwa zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), baadhi ya wadau wamejipanga kwa ajili ya kumchukulia fomu Rais wa sasa Wallace Karia, anayemaliza muda wake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Wadau hao wamejipanga kumchukulia fomu Karia majira ya saa 8 mchana, kwenye Makao Makuu ya TFF, kwa ajili ya kutetea kiti chake.

Licha ya Karia kuchukuliwa fomu, lakini alishaweka wazi nia yake ya kutetea kiti chake katika siku za hivi karibuni, mara baada ya kuongoza taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne.

Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Kiomoni Kibamba alishatoa ratiba la zoezi hilo, ambapo alisema kuwa uchukuaji wa fomu kwa nafasi ya Urais na kamati tendaji utaanza tarehe 8 mpaka 12 Juni, 2021.

Gharama za fomu kwenye nafasi ya Urais itakuwa shilingi 500,000, huku fomu kwa nafasi ya kamati ya utendaji zitatolewa kwa gharama za shilingi 200,000.

Uchaguzi huo mwaka huu utafanyika Jijini Tanga tarehe 7 Agosti, huku uongozi uliopo sasa chini ya Karia, ukimaliza muda wake katika kipindi cha miaka minne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!