October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wadau: Bajeti 2020/21 iguse maisha ya watu

Waziri wa Fedha, Dr Philip Mpango

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuja na bajeti itakayoziba mapengo yaliyoachwa na athari za mlipuko wa virusi vya corona (COVID-19), hususan katika uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na wadau mbalimbali akiwemo Dk. Hellen Kijo-Bisimba, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) wakati wakizungumza na Mwanahalisi Online.

Bajeti hiyo ni ya mwisho kwa utawala wa awamu ya tano ya Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ambaye aliingia madarakani tarehe 5 Novemba 2020.

Dk. Bisimba amesema bajeti hiyo inapaswa kuja  na mambo yatakayoleta ahueni kwa wananchi, baada ya kupata majeraha kutokana na corona.

Pia, inatakiwa kugusa mambo muhimu yanayohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Kuna mambo mengi ya kuangaliwa sababu pamoja na uchaguzi mkuu, tumepita kipindi kigumu cha Covid-19 ambayo imeathiri mambo mengi ya kiuchumi nchini. Kwa hiyo, inabidi hiyo bajeti iangalie itazibaje mapengo na mambo mengi yaliyoarthiriwa kiuchumi na covid-19,” amesema Dk. Kijo-Bisimba.

Dk. Helen Kijo Bisimba

Mwanaharakati huyo ameeleza, wananchi wanahitaji bajeti itakayogusa na kubadilisha maisha yao, na si vinginevyo.

“Wananchi wanategemea bajeti itakayosaidia kubadilisha maisha yao, itakayogusa vitu vya msingi na si bajeti itakayoleta machungu kwa wananchi.  Tunataka bajeti ambayo wananchi watafaidi, kama kwenye mambo ya kiuchumi,” amesema Dk. Kijo-Bisimba na kuongeza.

“Hususan kwa wakulima na wafugaji, inatakiwa kuangalia vitu vinavyowasaidia kupata pembejeo kwa wakati na masoko ili maisha yao yaende, na wafanyakazi hasa ambao mishahara yao imekuwa inachelewa, bajeti ikija isaidie kulipa madeni yao na kadhalika,” amesema

Mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Frank Festo anasema, “mimi natarajia bajeti iangalie zaidi katika sekta ya kilimo ili tusiwe na tatizo la chakula hasa kilimo cha umwagiliaji. Serikali itenge fedha za kutosha.”

“Bajeti ilenge kumunufaisha mwananchi, ni matumaini yangu kwamba, bajeti hii kwa kuwa ni ya mwisho ya Mheshimiwa Magufuli, itawajali moja kwa moja wananchi kama alivyowahi kusema kabla hajaondoka madarakani hatawaacha hivi hivi watumishi,” ameongeza

Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, John Minja amesema wanatarajia kuona, bajeti itakayosisimua uchumi hasa ambao hata kabla ya janga la corona kutokeam, “mwenendo haukuwa mzuri, tulihitaji bajeti itakayochachua uchumi.”

“Tunategemea bajeti itakayokwenda kuoneesha namna zile sekta zilizoathirika kwa kiasi kikubwa zikipewa ahueni. Mabenki yameendelea kutoza gharama za riba bila kujarisha kama kuna corona au la,” amesema

 Amesema, anatarajia bajeti hiyo kuongeza fedha katika sekta ya afya kutokana na hospitali zilizokuwa zikiwahudumiwa wagonjwa wa corona kutumia bajeti ambayo hawakuwa wameitarajia hivyo,  “Serikali iangalie uwasilishaji wa bajeti inayorudisha uimara wake.”

error: Content is protected !!