January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wachimbaji wanawake waiangukia serikali ada ya leseni

Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani, Asha Saidi akichekecha mchanga kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite

Spread the love

WANAWAKE wachimbaji wa madini wameiomba serikali ipunguze ada ya leseni ya uchimbaji madini ili kuwawezesha kinamama wanaoanza kazi hiyo ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za uchimbaji. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Wanawake hao waliounda Jukwaa la Kinamama wachimba Madini, wametoa kilio chao katika mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Hakimadini na kuwakutanisha wanawake wachimba madini kutoka mikoa ya Tanga, Singida, Manyara na Morogoro, uliofanyika mkoani Kilimanjaro.

Kinamama hao ambao wameamua kujikita kwenye shughuli za uchimbaji wa madini wameiomba serikali isikie kilio chao cha muda mrefu ili inawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Pili Hussein ambaye ni mwanamke wa kwanza kuchimba katika migodi ya Mirerani na kufanikiwa kiuchumi, amesema kuwa gharama kubwa za uendeshaji wa migodi zimekuwa kikwazo kwa wanawake hivyo ameiomba serikali na mashirika binafsi kujitokeza kuwasaidia.

Kwa upande wake, mchumbaji Mwansy Shomari kutoka machimbo ya Ruby mkoani Tanga amesema licha ya changamoto wanazozipitia mfumo dume umekuwa ukiwakwamisha kinamama kupiga hatua kiuchumi hususani katika sekta ya madini iliyotawaliwa na mfumo dume kwa kipindi kirefu.

Naye, Meneja Programu wa Shirika la Hakimadini, David Ntiruka amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kukusanya sauti ya kinamama wachimbaji pamoja na changamoto zao ili kuzifikisha kwenye vyombo husika viweze kufanyiwa kazi.

error: Content is protected !!