May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wachimbaji wadogo watakiwa kuongezea madini thamani

Spread the love

 

WACHIMBAJI wadogo wa madini nchini wametakiwa kufanya uchimbaji wa wenye tija na kuongeza thamani ya madini yao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa na Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko wakati akifungua mkutano mkuu wa 24 wa Chama cha Wanawake Wachimbaji wa Madini Tanzania (TAWOMA) uliofanyika jijini Dodoma.

Biteko amesema uchimbaji wa madini nchini unatakiwa kuzingatia sheria na taratibu ili kuongeza pato la taifa pamoja na mtu mmoja mmoja.

Katika ufunguzi huo, Biteko amesema katika masuala ya uchimbaji wa madini wanawake wanatakiwa kutambua kuwa ni haki yao kuchimba madini na kuachana na tabia ya kujidharau katika utendaji wao wa kazi.

Amesema katika kuboresha uchimbaji wa madini hususani wanawake, serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wanawake wachimbaji ili waweze kuboresha shughuli zao.

Amesema wanawake watashirikishwa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika sekta ya madini kwa nia kuboresha maisha ya wanawake na familia zao.

Aidha, Katibu wa Chama hicho, Salma Ernest amesema chama hicho kinakabiliana na changamoto ya kukosekana kwa umeme wa uhakika machimboni.

Salma amesema bado kuna changamoto ya uhaba wa masoko ya uhakika nchini na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kuchimbia madini.

Katika hatua ngingine, amesema TAWOMA wanamalengo ya kuwaunganisha wanawake wote nchini ili kufanya kazi kwa uhakika wa kibiashara.

Amesema wataanzisha mfuko wa pamoja wa wanawake ili kuwaweka pamoja na kuchochea maendeleo ya wanawake.

error: Content is protected !!