WACHIMBAJI wadogo wa madini wametakiwa kuzingatia taratibu za kitalaam wakati wa uchimbaji ili kuepuka ajali maeneo hayo, anaandika Mwandishi wetu.
Haya yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Charles Mlingwa wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), jijini Mwanza.
Amesema suala la usalama migodini ni muhimu na lazima lizingatiwe katika hatua za mwanzo za uchimbaji.
Amesema ni lazima kuchukua tahadhari katika maeneo ya migodini na kwamba wasiochukua hatua hizo za kulinda usalama serikali itaifungia.
Kwa upande wake Rais wa FEMATA, John Wambura amesema bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za elimu duni ya uchimbaji, uongezaj thamani na uchenjuaji wa madini.
Leave a comment