Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji madini wanawake wamlilia Magufuli 
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji madini wanawake wamlilia Magufuli 

Spread the love

WACHIMBAJI madini wanawake nchini wameitaka serikali kuwawezesha ili kukuza sekta hiyo inayochangia pato la taifa na kukuza ajira kwa vijana, anaandika Pendo Omary.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa warsha ya upatikanaji wa rasilimali zalishi- sekta za ardhi, madini na kilimo zilizofanyika wakati wa tamasha la jinsia la 14 ambalo limeandaliwa na asazi za kiraia, wanaharakati ngazi za jamii na kuratibiwa na TGNP- Mtandao.

Rachel Joseph, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake nchini (TAWOMA) ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online  anataka Rais Magufuli awasikie.

Amesema hakuna wanayeshindana naye duniani katika kuchimba madini ya Tanzanite na kwamba wanatakiwa kuchimba kidogokidogo wao  wenyewe.

Amehauri kuwa kwa sasa hakuna  haja ya kuleta wawekezaji kutoka nje, inachopaswa serikali ni kutuwezesha kwa kutupatia ruzuku ili wachimbe kisasa.

Rachel ambaye pia ni kati ya wanawake 30 wanaochimba madini ya Tanzanite Melelani amesema wanawake wachimbaji wanakabiliwa na chanagamoto zaidi kuliko wanaume hivyo wale wanaoweza vizuri kazi hiyo wanapaswa kuwezeshwa ili kuwachochea watoto wa kike kujiajili katika sekta hiyo ili kupunguza tatizo la ajira.

Aidha,   kwa upande wake Sarah Lusambagula, mvumbuzi wa madini ya kombati amesema suala la kupata vibali vya kuendesha shughuli hizo limekuwa ni changamoto.

“Tunapogundua maeneo yenye madini mara baada ya kufanya tafiti, tunalazika kuomba vibali serikalini, lakini tunachokumbana nacho huko ni rushwa na pale unaposhidwa kuwapatia lile eneo uliloligundua anapewa mtu mwingine licha ya kwamba ulikuwa na vigezo vya kupata leseni,” anasema Sara kutoka Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!