MMILIKI wa shamba lenye machimbo ya madini ya dhahabu, Iddrisa Hussein pamoja na wachimbaji wadogo wa eneo la Mahagi Kijiji cha Izunya Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wameiomba Serikali kufungua mgodi wao kuepusha maduara kujaa maji kutokana na jiografia ya eneo hilo. Anaripoti Paul Kayanda, Geita … (endelea).
Wachimbaji hao wamemuomba Afisa Madini mkazi wa mkoa wa Kimadini Mbogwe, Mhandisi Joseph Kumburu kutazama upya uamuzi wa kusitishwa kwa uzalishaji wa madini hayo.
Amesema badala yake awafungulie ili shughuli za uchimbaji ziendelee na serikali iweze kukusanya mapato yake huku wanakijiji nao wakinufaika na raslimali zilizopo kwenye eneo lao.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa mgodi wa Mahagi, Joseph Yabita amemuomba afisa madini huyo kuharakisha kufungua mgodi huo kwakuwa mwekezaji hana mgogoro na wamiliki wa mashamba pamoja na wachimbaji hao.
Leave a comment