May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wachezaji wa Simba wamvuruga kocha wao

Did Gomes kocha wa kikosi cha Simba

Spread the love

 

KUELEKEA mchezo wa marudiano dhidi ya Kaizer Chiefs, Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba, Didier Gomes ameshangazwa na wachezaji wake kwa kila mmoja kuwa na matamanio na hali ya kucheza mchezo huo kutokana na kuonesha viwango bora kwenye uwanja wa mazoezi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa hatua ya robo fainali utachezwa kesho majira ya saa 10 jioni, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Gomes ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, baada ya kutanabaisha kuwa katika mchezo wa kesho atakosa huduma ya Jonas Mkude, ambaye amepata matatizo ya kifamilia huku wengine waliobaki wakiwa na hali kubwa na kumuonesha utofauti kwenye mazoezi.

“Nimefurahishwa na mazoezi wiki hii nimewaona wachezaji wapya, kila mchezaji anataka kucheza huu mchezo wa robo fainali, tupo tayari kucheza isipokuwa mchezaji mmoja,” alisema kocha huyo.

Aidha Gomes aliongezea kuwa katika mchezo wa kesho watacheza zaidi ya uwezo wao licha ya kuwa wanacheza vizuri na watahakikisha wanatumia nafasi na kucheza kwa tahadhari kubwa.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Afrika Kusini kwenye Uwanja wa FNB, Simba ilipoteza kwa mabao 4-0, ili kufuzu hatua inayofuata inahitaji ushindi kuanzia bao 5.

Tayari Kaizer Chiefs wameshafika nchini wakiwa na kikosi cha wachezaji 23 huku kukiwa na ungezeko la mlinda mlango wao namba moja ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita.

error: Content is protected !!