KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi (Simba na Yanga) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa wachezaji wa timu zote mbili watapata nafasi ya kufturu wakati wa mchezo kutokana na baadhi yao kuwa kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhan. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utapigwa kesho majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa Habari Afisa Habri wa TFF, Clifford Ndimbo amesema mchezo huo umeangukia kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhan muda utakapofika mchezo utasimamishwa na wachezaji watapata muda wa kufturu kwa waliofunga.
“Wakati huu tupo kwenye mwezi wa Ramdhani na kuna wachezaji wapo kwenye mfungo kwa hiyo katika mchezo wa kesho kutakuwa na mapumziko mafupi ili kuwapa nafasi wachezaji na benchi la ufundi kupata futari,” alisema Afisa Habari huyo.
Aidha katika hatua nyingine Ndimbo, alisema mchezo wa kesho mageti ya uwanja huo yatafungwa majira ya saa 10 jioni, saa moja kabla ya mchezo ili kuepusha usumbufu na kuwataka mashabiki kuwahi mapema.
Leave a comment