October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wachezaji 13 kuwania tuzo Ligi Kuu 2020/21

Clatous Chama

Spread the love

 

JUMLA ya wachezaji 13 wamechaguliwa kuwania tuzo mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mimu wa 2020/21, katika vipengele tofauti tofauti. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Tuzo hizo ambazo zitatolewa Tarehe 21 Oktoba 2021 kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeeleza kuwa kwa mara ya kwanza zitatolewa tuzo binafsi 56, katika vipengele 42 vilivyoorodheshwa, ambazo ni tofauti zilizotajwa kwenye kanuni kwa timu washindi wa Ligi mbalimbali.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ kiungo wa klabu ya Yanga

Kipingere cha kwanza kuwaniwa kwenye tuzo hizo, kitakuwa mchezaji bora wa msimu, tuzo ambayo inashikiliwa na Clotous Chama mara baada ya kufanya vizuri kwenye msimu wa 2019/20, na mwaka huu atatetea tena tuzo hiyo mara baada ya kujumuishwa sambamba na Mukoko Tonombe wa Yanga na John Bocco wa Simba.

Kwa upande wa kipengere cha beki bora, wachezaji watakaowania ni Dikson Job ambaye alimaliza msimu akiwa na timu ya Yanga, sambamba na Mohammed Hussein na Shomari Kapombe kutoka klabu ya Simba.

John Bocco mshambuliaji wa Simba

Pia tuzo hizo kwa mara nyingine tena zitatoa mchezaji chipukizi aliyefanya vizuri, huku kwenye kinyang’anyiro hiko akiwekwa Lusajo Mwaikenda wa Kmc, Abdul Sopu wa Coastal union na Deogratius Mafie anayekipiga klabu ya Biashara United.

Waliotajwa kuwania kipa bora wa msimu ambao wanashindania ni Aish Manula kutoka Simba, Harun Mandanda wa Mbeya City na Jeremiah Kisubi ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Prison, ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Simba.

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

Vita nyingine itakuwa kwenye kipingere cha kiungo bora wa msimu, kipengere ambacho kimewajumuisha Clotous Chama, aliyekuwa anakipiga ndani ya klabu ya Simba, Feisal Salum na Mukoko Tonombe kutoka Yanga.

error: Content is protected !!