Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wachawi wamtisha Spika Ndugai
Habari Mchanganyiko

Wachawi wamtisha Spika Ndugai

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ameingia hofu kwa wachawi kukwamisha ujenzi wa daraja la Daraja la Kigongo Busisi, Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hivyo, muomba Mtemi Kafupa, Chifu wa eneo la Kigongo wilayani Misungwi, kuwashughulikia wachawi watakaojaribu kukwamisha ujenzi wa daraja hilo, unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Spika Ndugai ametoa ombi hilo leo tarehe 7 Desemba 2019, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja hilo, iliyofanyika eneo la Kigongo, jijini humo ambapo Rais John Magufuli ni mgeni rasmi.

Kiongozi huyo wa Bunge, amemueleza Mtemi Kafupa kwamba, anamuachia kazi ya kuhakikisha daraja hilo linajengwa.

“Mwanangu chifu wa eneo hili, Mtemi Kafupa nimefanya makusudi, tunakushuruku sana kwa salamu ulizotoa na kwa baraka ulizoto kwa daraja hili.

“Mimi ombi langu moja tu, wale wachawi watakaotaka kuchawia daraja hili lisijengwe. Washindwe kabisa, na hiyo kazi nakuachia wewe uhakikishe hili daraja linajengwa,” amesema Spika Ndugai.

Wakati huo huo, Spika Ndugai amempongea Rais Magufuli kwa uthubutu wake katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa madaraja, na kumuahidi kwamba Bunge linamuunga mkono kwa kila hatua.

“Tunakushukuru kwa kazi hii hii,  ni historia kubwa ya kujiamini kwa nchi yetu kama rais anavyotuambia kwamba Watanzania tunaweza. Ujenzi wa daraja hili unathibitisha maneno yako kwamba tunaweza,” amesema Spika Ndugai na kuongeza;

“Ni uthubutu wa hali ya juu tunapokaribia kufikisha miaka 60 ya uhuru wetu,  ndipo tunapoweza kufanya miradi mikubwa kiasi hiki chini ya uongozi wako. Bunge tunakuunga mkono katika hili, tutajitahidi katika kutenga fedha na bajeti kuhakikisha mradi huu unakamlika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!