April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wabunifu mavazi Tanzania wajitosa vita ya corona

Spread the love

CHAMA kinachoshughulikia na masuala ya ubunifu wa mavazi, Fashion Association of Tanzania (FAT), kimejitosa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jana Jumatano tarehe 6 Mei 2020, chama hicho chenye wanachama zaidi ya 60, kimemkabidhi Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katoni 80 za vitakasa mikono, zenye thamani ya Sh. 2 milioni.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mustafa Hassanali, Mwenyekiti wa TAF, amesema mchango huo umetolewa kwa ajili ya kusaidia kudhibiti maambukizi ya COVID-19.

Fashion Association of Tanzania (FAT) chaendesha mchakato wa uchangiaji wa vitakasa ikiwa sehemu ya mchango wao dhidi ya maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona (Covid-19).

“Wanachama wa FAT pamoja na wadau wengine wa tasnia ya ubunifu wa mavazi na mitindo wenye mapenzi mema na Tanzania wametoa michango yao iliyofanikisha upatikanaji wa vitakasa hivi, ili kuhakikisha vinapatikana kwenye jamii, kwa ajili ya mapambo dhidi ya COVID-19,” amesema Hassanali.

Aidha, Hassanali amewataka Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuwa ni hatari kwa afya zao, ikiwemo kufuata ushauri wa watalaamu wa afya juu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya COVID-19.

Ugonjwa wa COVID-19, kwa mara ya kwanza uliripotiwa nchini mwezi 16 Machi 2020, ambapo hadi sasa serikali imengaza watu 480 kwamba wameambukizwa ugonjwa huo, huku vifo vikiwa 16.

error: Content is protected !!