June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge waumbuana bungeni

Mbunge wa Msoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere

Spread the love

MBUNGE wa Msoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema) amempa wakati mgumu Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeti Mbene kwa kumtaka kuthibitisha kauli yake bungeni kuwa, Serikali ya CCM imewadhulumu waliokuwa wafanyakazi wa viwanda vya nguo vya Mutex na Mwatex. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Nyerere alitoa kauli hiyo leo bungeni alipouliza swali la nyongeza kuhusu ulipwaji wa wafanyakazi waliokuwa katika viwanda hivyo jambo lililomfanya Mbene ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa kuyumba.

“Mheshimiwa Spika naomba kuuliza swali dogo la nyongeza, jana wakati naongea na Naibu Waziri juu ya malipo kwa waliokuwa wafanyakazi wa viwanda vya nguo vya Mwatex na Mutex, alisema kuwa serikali imewadhulumu watu hao.

“Sasa naomba Naibu Waziri awadhibitishie wafanyakazi hao maneno aliyoniambia kuwa, Serikali ya CCM imewadhulumu wafanyakazi hao kama alivyoniambia mimi,” amesema Nyerere.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Mashashanga (Chadema) alitaka kujua ni kwanini kiwanda cha DAHONG Textile Com Ltd kilichopo katika Halmashauri ya Shinyanga kimekuwa hakitengenezi nguo kama mkataba unavyohitaji.

Akijibu maswali hayo Mbene amesema, si kweli kuwa serikali imekusudia kudhurumu waliokuwa wafanyakazi wa viwanda hivyo ingawa wapo wanaodai kupunjwa katika malipo hayo.

“Nikweli jana wakati naongea na Mheshimiwa Nyerere tulikuwa tukiongea tena yeye aliniuliza kwa mzaha kuwa, Serikali ya CCM imeamua kuwadhulumu wafanyakazi hao na mimi nilimjibu kuwa kama yeye anaona tumewadhulumu basi tumewadhulumu,” alijitetea.

Mbene amesema, usajili wa kiwanda hicho unaelekeza kuzalisha nyuzi na si kuzalisha nguo kama ilivyo hoja ya mbunge.

Amesema, kiwanda hicho kimewekeza mtaji wa Dola za Marekani milioni 66.4 sawa na Sh. Bilioni 150 na kina ajiri Watanzania wapatao 330 ambapo kinatarajia kuzalisha tani 6,000 za nyuzi kwa mwaka.

error: Content is protected !!