Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge watembelea pori la akiba Kilombero, waahidi ushirikiano kulinda mazingira
Habari Mchanganyiko

Wabunge watembelea pori la akiba Kilombero, waahidi ushirikiano kulinda mazingira

Spread the love

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema pori la Akiba Kilombero ni chachu ya kufungua fursa za utalii ikiwemo shughuli za uwindaji wa kitalii ambazo zinaongeza fedha nyingi za kigeni nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza wakati wa kutoa wasilisho mahsusi la Pori la Akiba Kilombero, kwenye semina kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma juu ya Usimamizi wa Pori la Akiba Kilombero, Kamishna wa Uhifadhi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Joas Makwati alisema pori la hilo kwa sasa lina vitalu vinne vya uwindaji wa kitalii.

Makwati alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi 2020/21 TAWA ilitoa jumla ya Sh. 425.2 milioni kwa Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi kama gawio la 25% ya mapato yatokanayo na shughuli za utalii katika Pori la Akiba Kilombero.

Alisema Pori hilo lina umuhimu mkubwa kwa Taifa kwani linachangia asilimia 65 ya maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere (JHPP) ambayo yanatarajia kuzalisha Megawati 2,115 za umeme utakaotumika majumbani, viwandani na kwenye shughuli za usafirishaji (reli na magari).

Pamoja na faida zingine Makwati alisema TAWA imetoa fursa Kwa wananchi kufanya shughuli za uvuvi kwa utaratibu maalumu katika pori hilo, jambo ambalo limewanufaisha sana wakazi kwa Kilombero na mkoa wa Morogoro kwa ujumla.

Akibainisha changamoto za pori hilo, Kamishna Makwati alisema pori hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi ambapo kwa sasa kuna jumla ya watumishi 88 kati ya watumishi 279 wanaohitajika pamoja na ukosefu wa miundombinu.

Akieleza hatua za kukabiliana na changamoto hizo, Makwati alisema TAWA imeandaa mpango shirikishi wa Miaka mitatu (2023 – 2025) wa usimamizi wa pori hilo utakaohakikisha ulinzi, uhifadhi, na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na Wanyamapori unafanikiwa.

Pia TAWA imeongeza vitendea kazi (gari 05, boti 04, trekta 02, na pikipiki 02), imeanzisha kanda mbili za kiutawala ili kuimarisha ulinzi na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi na usimamizi wa pori.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Anderson Mutatebwa ametoa ufafanuzi wa kisera kuhusu tathmini inayofanywa na Serikali kwa wananchi wa Kijiji cha Ngombo na vitongoji vilivyopendekezwa kuondolewa nje ya hifadhi.

Naye Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi Nyanda alisema kuhusu suala la matumizi bora ya ardhi, utekelezaji wake unahitaji ushirikishwaji wa kutosha kwani ni suala mtambuka ambalo litahusisha wadau mbalimbali na sekta za Serikali ikiwemo wizara ya TAMISEMI, ambapo ameomba kuongeza umoja na mshikamano katika suala hilo ili kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuridhia kuanzisha pori la akiba Kilombero na kuahidi kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na kamati za Bunge, wabunge wa maeneo husika, Serikali za mkoa na Wilaya, pamoja na wananchi ili kufikia malengo ya uhifadhi endelevu kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya Umma, Augustino Vuma ameeleza kufurahishwa kwake na wasilisho la pori la akiba Kilombero na kusema kuwa kamati imelielewa na hivyo watajitahidi kuonesha ushirikiano wao kwa TAWA ili kuhakikisha inaendelea kulinda mazingira na rasilimali zilizopo ndani ya hifadhi hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!