Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge watatu Upinzani kutua CCM kabla Bunge kuanza
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge watatu Upinzani kutua CCM kabla Bunge kuanza

Spread the love

WABUNGE watatu wa upinzani- wawili Chadema na mmoja Chama cha Wananchi (CUF), wako mbioni kuvikimbia vyama vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Habari kutoka kwa watu waliokaribu na wabunge hao na CCM zinasema, tayari mazungumzo ya kuwachukua wabunge hao tayari yamekamilika.

“Hawa wawili wataondoka wakati wowote. Tayari wameomba na kukubaliwa kujiunga na CCM. Huyu mmoja ameomba ashiriki mkutano huu wa Bunge ili aweke mambo yake, ikiwamo kuaga wabunge wenzake,” ameeleza kiongozi mmoja wa CCM kwa sharti la kutotajwa jina.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, wabunge wanaotaka kuondoka, wametaja sababu tofauti. Hakuzitaja.

MwanaHALISI Online inaendelea kufuatilia undani wa suala hilo na litaanika jina la kila mbunge na hata mpanga mkakati mwenyewe.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja takribani mwezi mmoja tangu wabunge wengine wawili wa Chadema na mmoja wa CUF, kuvihama kwenye vyama vyao.

Wabunge walindoka Chadema, ni Mwita Mwaikabe Waitara (Ukonga) na Julius Kalanga (Monduli).

Kwa upande wa CUF, mbunge aliyehama na kujiunga na CCM, ni Zuber Mohammed Kuchauka (Liwale).

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho kumeongezeka wimbi la madiwani wa upinzani kuondoka kwenye vyama vyao na kujiunga na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao watatu, wameamua kuvihama vyama vyao kwa sababu zinazolingana.

“Wote watatu wanaondoka siyo kwa sababu wanaunga mkono juhudi, bali wanaondoka kutokana na matatizo wanayodai yapo kwenye vyama vyao,” ameeleza mmoja wa viongozi wa CCM aliyeshiriki mpango wa kuwachukua wabunge hao.

Anasema, mpango uliyopo mmoja wa wabunge anatarajiwa kuhama katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!