January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya elimu waja na mwarobaini wa ajira

Spread the love

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Tanzania imeandaa mkakati wa kitaifa wa maendeleo ya stadi za kazi kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana. Anaadika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Elimu ya Juu (WEMU), Dk. Jonathan Mbwambo katika mkutano na waanahabari Jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya mkakati huo.

Mpango huo utatarajiwa kutekelezwa ifikapo mwaka 2016/17-2025/26 katika kuboresha maendeleo ya stadi za kazi zinazoendana vitendo.

Mbwambo amesema kuwa mipango hiyo ya maendeleo ya stadi za kazi imeandaliwa kwa kuzingatia kipaumbele cha sekta ya kilimo, biashara, utalii, uchukuzi, ujenzi, nishati pamoja na TEHAMA.

Amesema kuwa ili kuwezesha utekelezaji wa mikakati hiyo kwa kuzingatia sekta husika, masuala ya jumla ya utaratibu za ugharamikaji na utawala yamewekwa kwenye mkakati huo.

Mbwambo amesema kuwa pamoja na vipaumbele vilivyoweka kwenye mkakati, serikali imepanga kuandaa wataalam wakutosha katika ngazi zote za mafundi wa ngazi ya kati na juu na kupanua mafunzo ya ngazi zote ya wahandisi, mafundi mchundo, kuandaa mfumo wezeshi wakuhakikisha kila kampuni ya kigeni ya ujenzi inakuwa na wakufunzi ili kuhamisha utaalam wa Watanzania.

“Utafiti unaonyesha vijana 14,000,000 nchini Tanzania hushindwa kupata ajira na kipato cha uhakika kutokana na changamoto mbalimbali za stadi za maisha hivyo inahitaji kuwa na rasilimali watu wenye ubora wa hali ya juu katika ngazi ya chini, kati na juu kabisa ili kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” amesema Mbwambo.

Pamoja na vipaumbele hivyo vinavyoandaa ajira kwa vijana, Mbwambo amesema, shughuli zote ziendeshwe kwa kushirikisha wadau wote ili kuondokana na mfumo wa kila sekta kufanya mafunzo bila kuhusisha sekta nyingine.

error: Content is protected !!