July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge watakiwa kuweka maslahi ya Taifa mbele

Spread the love

CHAMA cha Wakulima Tanzania (AFP) kimewataka wabunge wanapokuwa bungeni waweke maslahi ya taifa mbele badala ya kupigania vyama vyao. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Afisa Mahusiano wa chama hicho, Peter Sarungi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuwa wabunge wengi wamekuwa na utamaduni wa malumbano yasiyokuwa ya msingi kutokana na maslahi ya vyama vyao, na kuacha jambo la msingi ya kutetea maslahi ya taifa.

Sarungi amesema kuwa wabunge wengi wamekosa uzalendo ambapo inashiria kuwa wao siyo wajenzi wataifa bali ni wajenzi wa vyama vyao, kitu ambacho kinawaweka wananchi waliowachagua kukosa uwakilishi hai bungeni.

“Waheshimiwa wabunge wanakwenda na kasi ya zaidi ya kusimamia vyama vyao kuliko masuala maalu ya kitaifa,” amesema Sarungi.

Sarungi amesema kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wagombea wanane kwenye nafasi ya uspika bungeni lakini hakufanikiwa kuchaguliwa ambapo wabunge hupigia kura mgombea wa chama chao hata kama hana sifa ili kuendeleza maslahi ya chama na sio Watanzania.

error: Content is protected !!