Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wataka ruzuku iwekwe, tozo ziondolewe kuhimili bei ya mafuta
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wataka ruzuku iwekwe, tozo ziondolewe kuhimili bei ya mafuta

Spread the love

 

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameishauri Serikali kuondoa tozo zisizo na athari katika miradi muhimu kwa wananchi pamoja na kuweka ruzuku katika mafuta ya taa, petrol na dizeli ili kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa hiyo adimu duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo tarehe 5 Mei, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati wakichangia hoja ya kupanda kwa haraka kwa bei ya mafuta hayo iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omary Kigua (CCM).

Kigua amesimama bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 54 na kuliomba Bunge liahirishwe kwa dharura kujadili taharuki ya bei hiyo ya mafuta nchini.

Baada ya Spika Dk. Tulia Ackson kuungana na wabunge kukubaliana na hoja hiyo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma amekuwa wa kwanza kushauri kwamba Bunge liishauri Serikali iondoe tozo kadhaa ambazo ni kati ya tozo zaidi ya 23 zilizopo katika mafuta hayo ili kushusha bei ya mafuta.

Msukuma ambaye amesema lita moja ya mafuta ya dizeli katika jimbo lake inauzwa Sh 5,000, pia ameitaka Serikali ikope kufidia gharama za bei hiyo bidhaa hiyo.

Hoja ya Msukuma iliungwa mkono na Mbunge wa Busega, Simon Songe (CCM) ambaye naye ameishauri Serikali itafute fedha na kupeleka ruzuku kwenye mafuta ili kupunguza gharama za bidhaa hiyo.

“Kuna tozo nyingi tumeweka kwenye mafuta kuna haja ya kuangalia baadhi ya tozo hizi tuziondoe kwa wakati huu wa dharura yaani Mei na Juni. Tozo hizo zitafikia kama Sh 400 hadi 500 na hamna namna tunavyoweza kufanya kwa sababu maisha yanategemea mafuta,” amesema.

Aidha, Mbunge wa Madaba, Joseph Mhagama (CCM) amesema kuanzia Januari, 2021 hadi Mei, 2022 mafuta petroli yamepanda kwa asilimia 92.

Amesema mafuta yalipanda kutoka Sh 1,695 mwaka 2021 hadi zaidi ya Sh 3,000 mwaka huu jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa watanzania.

“Katika miezi hii miwili Aprili na Mei, mafuta yamepanda kwa asilimia 21, gharama ya maisha kwa watanzania imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 92 kati ya 2021, 2022,” amesema.

Mbunge huyo ameshauri Serikali ikubali kuondoa tozo mbili ambazo ni fuel levy (ushuru wa barabara) na excise duty (Ushuru wa bidhaa) ambazo zinachangia karibu Sh 792 kwenye bei ya mafuta.

Aidha, Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM) naye ameishauri Serikali itumie mbinu iliyotumiwa na Serikali ya Kenya kwa kukopa fedha kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) zaidi ya Sh bilioni 900 na kuweka ruzuku kwenye mafuta kiasi cha kusaidia kushusha bei ya mfuta nchini humo.

Hata hivyo, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), amesema Serikali hailali katika kushughulikia jambo hilo.

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

“Tunahitaji kutafakari kwa uangalifu mkubwa, mambo yapo kwa mujibu wa sheria, tukienda kwa fujofujo tunaenda kuathiri ya maji, tarura, reli hivyo lazima tuangalie hayo. Tukikurupa tutaharibu mambo mengine,” amesema.

Wakati Waziri wa nishati, Januari Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli, mbali na kufafanua kwa kina sababu za kupanda kwa bei ya mafuta hayo duniani, amesema; “Niwahakikishie wabunge kwamba serikali inawajali wananchi wake, inajua kilio chao hivyo tunachukua ushauri wenu na kwenda kuufanyia kazi.”

Akijumuisha michango ya wabunge 17 waliochangia hoja hiyo, Spika Dk. Tulia amesema Bunge linampa Waziri Makamba muda wa siku tano hadi Jumanne wiki ijayo ili aje na kauli ya Serikali kuhusu suala hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

error: Content is protected !!