SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kutovaa tai nyekundu, bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Ni leo Alhamisi saa 10:00 jioni, tarehe 22 Aprili 2021, wakati Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atakapokwenda kulihutubia Bunge hilo.
Rais Samia, anakwenda kuhutubia Bunge kwa mara ya kwanza, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Hayati John Pombe Magufuli, aliyefariki 17 Machi 2021 na mwili wake, kuzikwa Chato mkoani Geita.

Akitoa tangazo hilo leo asubuhi, Spika Ndugai amesema, kukiwa na kiongozi mkubwa wa nchi anapokwenda kuhutubia Bunge, tai nyekundu inayoonyesha mamlaka inavaliwa na mtu mmoja pekee
“Tai nyekundi ni ya mamlaka, inapaswa kuvaliwa na mtu mmoja tu. Jioni msije mmevaa tai nyekundi, mtarudia getini,” amesema Spika Ndugai huku wabunge wakishangilia.
Leave a comment