Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wambana Dk. Tulia Bunge kumezwa na Serikali
Habari za Siasa

Wabunge wambana Dk. Tulia Bunge kumezwa na Serikali

Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

MGOMBEA wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amewahakikishia wabunge kuwa Bunge halitamezwa na Serikali licha ya uwingi wa wabunge wa chama tawala – CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Tulia ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Februari, 2022 wakati akiomba kura kwa wabunge kuchaguliwa katika nafasi hiyo ya Spika.

Dk. Tulia alikuwa akijibu maswali ya wabunge Mrisho Mgambo wa Arusha Mjini (CCM) na Aida Khenani wa Nkasi Kaskazini (Chdema)

Gambo amehoji kwamba kwa kuwa Bunge lina wabunge wengi wa CCM, wananchi wanaamini ni rahisi Bunge kumezwa na serikali, Je, akikuchagua unawahakikishiaje kwamba atalinda heshima ya Bunge ndani na nje ya Bunge.

Wakati Khenani amemhoji kwamba amejipangaje kulinda heshima na hadhi ya Bunge kwa kuwa kumekuwa na mazingira nje ya Bunge kuwa Serikali inaingilia mhimili huo.

Akijibu maswali hayo, Dk. Tulia amesema kwa muktadha wa majukumu ya wabunge, Bunge ni muhimili ambao umepewa kazi kikatiba wa kuisimamia na kuishauri serikali.

Amesema haijalishi ni mbunge wa CCM au upinzani, yeyote atakayeleta hoja atapewa fursa kwa sababu mbunge ni mwakilishi wa wananchi.

Amesema licha ya wabunge wengi kuwa CCM, Bunge haliwezi kumezwa na Serikali.

“Huo uwezekano haupo kwa sababu Bunge haliwezi kumezwa na Serikali wala muhimili mwingine.

“Serikali kazi yake ni utendaji na Bunge ni kuisimamia Serikali kuhakikisha je, kutenda kwake kunaleta maendeleo kwa wananchi au hapana,” amesema.

Aidha, amesema ushirikiano kati ya serikali na Bunge, mihimili mingine hauna tatizo.

Amesema kwa miaka sita ambayo amekuwepo bungeni hakuna mazingira yoyote ambayo serikali iliingilia Bunge katika shughuli zake au Bunge kuingilia muhimili mwingine.

Amesema Bunge litaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na sheria walizojiwekea wenyewe.

“Nieleze watu wafahamu kuwa Bunge tumepewa kazi zetu, sisi ni daraja kati ya wananchi na serikali, kazi yetu ni kuhakikisha serikali inapeleka maendeleo kwa wananchi, wakati huohuo daraja liwezeshe mawazo ya wananchi changamoto lazima ziifikie serikali.

“Niwatoe hofu wananchi kwamba Bunge litaendeshwa kwa namna Fulani hapana!, hakuna unyonge mahali popote.

“Wabunge ambao mmeliwachagua wanao uwezo wa kuisimamia, kushauri, kuwajibisha serikali pale itakapohitajika,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema ataliongoza Bunge kuhakikisha wabunge mnapata fursa ya kuihoji serikali kwa heshima, busara na kwa kufuata kanuni zetu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!