Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waliofukzwa Chadema watinga bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge waliofukzwa Chadema watinga bungeni

Spread the love

 

BAADHI ya Wabunge wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametinga bungeni siku moja baada ya Baraza Kuu la chama hicho kutupilia mbali rufaa zao za kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wabunge 19 wa viti maalumu walifukuzwa Chadema tarehe 27 Novemba 2020 na kamati kuu ya chama hicho wakituhumiwa kughushi nyaraka za chama, usaliti na kisha kujipeleka bungeni jijini Dodoma kujiapisha kuwa wabunge wa viti maalum.

Baada ya kufukuzwa, walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho lililokutana juzi Jumatano tarehe 11 Mei 2022 na kumalizika jana pamoja na mambo mengine lilisikiliza rufaa zao na kuzitupilia mbali kwa kura 413 kati ya 423 zilizopigwa na wajumbe.

Wabunge hao wameingia bungeni leo Ijumaa tarehe 13 Mei 2022 na baadhi yao akiwemo Esther Matiko na Salome Makamba wameuliza maswali katika kipindi cha maswali na majibu.

Wakati wabunge hao wakiingia bungeni chama chao kimesema leo kuwa, kimewasilisha barua kwa Spika wa Bunge kumweleza kuhusu hatima ya rufaa za waliokuwa wanachama wao, Halima Mdee na wenzake 18.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter.

“Barua kuhusu Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama 19 @ChademaTz imeshafika kwa Spika.”

“Hii ni barua ya pili baada ya ile ya kufukuzwa kwao uanachama na Kamati Kuu mwaka 2020. Spika ni vyema akaheshimu na kutekeleza sasa matakwa ya katiba ya nchi na sheria,” amesema Mnyika

Tarehe 14 Februari 2022, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma alisema Mdee na wenzake wako bungeni kihalali.

Alisema hayo wakati akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua uhalali ama uhalamu wa wao kuendelea kuwa bungeni licha ya kufukuzwa ndani ya chama chao.

Dk. Tulia aliyekuwa na siku chache tangu kuwa Spika akichukua nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu tarehe 6 Januari 2022 alisema, Bunge halioni shida kuwaondoa wabunge na lilishawahi kufanya hivyo katika mabunge yaliyotangulia.

“Jambo linalosubiriwa ni kumaliza michakato yao ya ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua,” alisema Dk. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini.

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa.

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!