July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge walalamikia fedha mfuko wa vijana

Spread the love

Na Dany Tibason

SUZAN Kiwanga, Mbunge wa Jimbo la Mlimba (Chadema) leo bungeni amelalamika kwamba, fedha zinazotengwa kwa ajili ya kusaidia vijana kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana katika Halmashauri ya Wilaya Morogoro, haziwafikii.

Malalamiko hayo pia yametolewa na Mgumba Omary ambaye ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM) aliyehoji serikali kuwa, inachukua hatua gani ile fedha za vijana wa vijiji vyote 64 vya jimbo lake ziweze kuwafikia ili kupunguza chanagmoto ya ajira.

Wabunge hao wametoa malalamiko hayo leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

“Hizi fedha haziwafikii vijana, serikali ina mpango gani wa kuhakikisha sasa fedha hizo zinawafikia walengwa,” amehoji Kiwanga.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Sulemani Jaffo amesema, tayari serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuwawezesha vijana.

Jaffo ameeleza kuwa kila halmashauri zinatakiwa
kutenga asilimia tano ya mapato yake ya ndani kila mwaka wa fedha kwa ajili ya vijana.

Hata hivyo, amesema katika bajeti ya mwaka 2014/2015 Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro  ilifanikiwa kutoa Sh. 10.3 milioni kwa vikundi 19 vya vijana kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Katika bajeti ya mwaka 2015/2016 vikundi vya vijana vimetengewa Sh. 87.5 milioni ili kuviwezesha kiuchumi na hatimaye kujiajiri.

Amesema, mpango huo ni endelevu na katika bajeti ya mwaka 2016/2017 halmashauri

inakusudia kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya kufyatulia tofali ili ziweze kuwanufaisha vijana wengi zaidi kiuchumi na kuboresha makazi yao.

error: Content is protected !!