Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waivaa Serikali ndoa za utotoni
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge waivaa Serikali ndoa za utotoni

Wasichana waliopata mimba za utotoni
Spread the love

 

MJADALA wa mtoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18 haujapoa. Ndivyo unaweza kusema baada ya suala hilo kuulizwa bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Kwa kipindi kirefu, mjadala huo umekuwa ukiibuka hasa ikizingatia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa amri ya kufanyika kwa marekebisho ya sheria hiyo ili iendane na Katiba ya Tanzania kwamba mtoto aolewe akiwa na umri zaidi ya miaka 18.

Leo Jumatano tarehe 8 Septemba 2021, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Zainabu Katimba ameuliza swali bungeni akisema ni lini serikali ya italeta muswada wa sheria ya ndoa bungeni ili kurekebisha vifungu vya sheria vinavyohusu mtoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18.’’

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda amesema, muswada huo wa sheria ya ndoa ulifikishwa kwenye kamati ya katiba na sheria Februari 2021, kufuatia uamuzi ya Mahakama ya Rufani katika kesi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi Rebecca Gyumi, Rufaa Na.204/2017 na Na.5/2016 ya Mahakama Kuu iliyotaka sheria ya ndoa ifanyiwe marekebisho ili mtoto wa kike aolewe akiwa na miaka 18.

“Kamati baada ya mapitio iliona upo uhitaji wa kushirikisha wadau wengi zaidi ili kupata maoni zaidi,” amesema Pinda

Amesema, Serikali inaendelea na zoezi la kushirikisha wadau ambapo hadi sasa Serikali imefanya mkutano na viongozi wa dini katika mkoa wa Dar es Salaam tarehe 17 Machi, 2021.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Zainabu Katimba

Amesema, mkutano wa pili ulifanyika jijini Dodoma tarehe 2 Julai, 2021 uliojumuisha wabunge wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wa Halmashauri ya Mkoa wa Dodoma.

Pinda amesema, kurejeshwa kwa muswada huo serikalini kulitokana na unyeti wa jambo lenyewe.

“Nipende kumuarifu mbunge kuwa, Serikali itakapokamilisha michakato iliyoelekezwa na kamati ya Bunge, muswada huu utawasilishwa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kisha kuwasilisha mbele ya Bunge kwa ajili ya kutunga sheria husika,” amesema.

WANAHARAKATI WASHANGAA KIGUGUMIZI CHA SERIKALI

Majibu hayo yameifanya MwanaHALISI Online kuzungumza na wadau mbalimbali kuhusu suala hilo ambapo, Mkurugenzi mtendaji Taasisi ya msichana initiative, Rebecca Gyuni aliyeshinda kesi hiyo, amesema tangu Oktoba 2019, serikali ilipewa muda wa mwaka mmoja kwenda kutekeleza uamuzi wa mahakama lakini anashindwa kuelewa kwanini hadi sasa Serikali inapiga danadana kutekeleza uamuzi huo.

Rebecca amesema, serikali inapoendelea kuchelewa kutekeleza uamuzi wa mahakama, inamweka mtoto wa kike kwenye mazingira magumu ya kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18.

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Msichana Initiative, Rebecca Gyuni

“Sijajua kwa nini Serikali inachelewa kwani maelekezo yako wazi na serikali ilitakiwa itekeleze ndani ya mwaka mmoja. Nampongeza mbunge Zainabu kwa kutekeleza wajibu wake kwa kuisimamia serikali,” amesema Rebecca.

Alipoulizwa mikakati gani wanaifanya, Rebecca amesema “tumekuwa tunafanya mikutano ya moja kwa moja na wabunge kupitia kamati ya katiba na sheria na niseme tu, mwamko wa wabunge ni mkubwa na hawajui kwa nini serikali wamechelewa kuuleta.”

Aidha, kwa upande wake mmoja wa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Felister Mauya naye aliungana na Rebecca na kuwataka wabunge na wanasiasa wengine kutumia wajukwaa yao kuishinikiza serikali itekeleza uamuzi wa mahakama mapema ili kunusuru watoto wa kike wanaolewa chini ya umri wa miaka 18.

Alisema licha ya kwamba ni kweli kuwa walishirikishwa katika kutoa maoni kwenye kamati hiyo ya bunge na katiba na sheria, bado wanaishangaa serikali kwanini imekuwa na kigugumizi kutekeleza hukumu hiyo ya mahakama kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!