July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge waipigia debe Zanzibar Fifa

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia

Spread the love

SAKATA la Zanzibar kujiunga na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) limetinga bungeni, baada ya wabunge waitaka serikali kuiomba uachana Zanzibar. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) alipoitaka serikali kuiandikia Fifa, iweze kuwapatia uanachama Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kama ilivyo kwa Hong Kong.

Murtaza aliuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa kutatua mgogoro kati ya Shirikisho la Mira wa Miguu Tanzania (TFF) na ZFA umekuwa wa muda mrefu sana ambapo ZFA ikitaka kuingia katika uanachama wa FIFA.

“Je, nijitihada gani ambazo zinafanywa na serikali za kuiandikia FIFA ili ZFA iweze kupata uanachama kama ilivyo Hong Kong?” alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema huo si mgogoro bali ni kupishana kwa lugha kati ya ZFA na TFF.

Alisema TFF imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba ZFA inapata uanachama kama ilivyokuwa katika Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na ndiyo maana inashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hivyo sioni kama kuna dhambi kama TFF ikiishauri FIFA ili ZFA ipate uanachama shirikishi kwenye shirikisho hilo na sisi serikali tutashirikiana nao,” amesema.

error: Content is protected !!