SERIKALI kwa kumtumia Wakala wa majengo (TBA) imeanza upembuzi yakinifu wa majengo yatakayofanyiwa ukarabati pamoja na yale yatakayobomolewa na kujengwa upya, Anaripoti Victoria Mwakisimba TUDARCo … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma leo tarehe 10 Septemba 2021 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM, Alice Kaijage.
Mbunge huyo amehoji kwamba “je serikali ina mpango gani wa kukarabati hospitali ya wagonjwa wa afya ya akili ya Mirembe ambayo miundombinu yake imeharibika.
Akijibu swali hilo Dk. Mollel amesema ni kweli utafiti wa awali kuhusu gharama zitakazotumika kufanya ukarabati wa hospitali hiyo umekamilika hivyo serikali itaanza utekelezaji wa mpango huo, kazi hii inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwa mwezi Oktoba,2021.
Kwa upande wa Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye amehoji, serikali ina mpango gani juu ya ujenzi wa kituo cha afya katika jimbo la Mtama ambacho naibu waziri alitembelea na kuona hali yake.
Akitoa majibu naibu waziri wa afya amesema ni kweli alizuru jimboni humo na kuona hali ya wananchi wa Mtama wanavyopata adha, amesema kuwa serikali imetenga milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Leave a comment