January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge waibana serikali sekta ya afya

Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge ya Huduma za Jamii, Lediana Mng'ong'o (CCM)

Spread the love

BUNGE limeelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni 2.7 nchini, wanakabiliwa na udumavu kutokana na ukosefu wa lishe bora. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Takwimu hizo, zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge ya Huduma za Jamii, Lediana Mng’ong’o (CCM) wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Amesema takwimu kutoka Shirika la Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), zinaonesha kuwa watoto wa hao wanakabiliwa na tatizo la kudumaa hali ambayo ni hatari kwa Taifa.

Mng’ong’o amesema takwimu hizo zinaonesha kila watoto 100 mkoani Kagera, 52 wanakabiliwa na tatizo hilo, sawa na asilimia 52 na mkoa wa Iringa kila watoto

100, watoto 51 wamedumaa sawa na asilimia 51.

Amefafanua kuwa, hali hiyo ya kudumaa pia ipo katika mkoa wa Njomnbe, Rukwa na kwingine nchini na kwamba inaweza kusababisha Taifa kukosa watoto wenye sifa za kutumikia Taifa.

“Takwimu zinaonesha kuwa mkoa wa Iringa na Njombe ni mikoa ambayo inakabiliwa na changamoto ya uwepo wa watoto waliodumaa lakini pia hata maambukizi ya virusi vya Ukwimu yapo juu, hivyo ni vema kuwepo mkakati wa pamoja wa kupunguza hali hiyo. Kwanini kila siku sisi,”Amehoji.

Amesema kuwa, kutokana na hali hiyo, kuna dalili kwa Taifa kukosa wataalam wa sayansi kwani uwezo wao utakuwa mdogo katika kufikiri na kufanya maamuzi.

Kuhusu ongezeko la Ukimwi, Mng’ong’o amesema linahitaji ushirikishwaji wa pamoja kwani kuachia asasi za kiraia itachukua muda kukabiliana na tatizo hilo, pia ni sababu ya kusambaa nchini.

Ameitaka wizara kuhakikisha inatoa fedha katika vituo vya afya na zahanati ambazo wananchi wamejitolea kujenga ili viweze kutoa huduma bora.

Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM), ameitaka serikali kutoa fedha ili kuhakikisha miradi na madeni ya wafanyakazi wa hospitali ya Rufaa Dodoma yanalipwa.

Bura amesema hospitali hiyo imepewa sifa ya rufaa lakini hakuna kinachofanyika chenye sifa ya rufaa, jambo ambalo linakatisha tamaa wananchi wa mkoa huo.

Naye mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage (CCM), amesema serikali imeitelekeza hospitali ya mkoa huo ya Kitete ambapo huduma muhimu kama X-ray haipatikani mkoani kote.

Ameipongeza serikali kwa kuhakikisha kuwa magari ya kubebea wagonjwa yamepatikana mkoa wote lakini akashauri ziwepo pia huduma za uhakika.

Conchester Rwamlaza (Chadema), amesema serikali imekuwa ikifanya mambo bila kupanga ambapo hata utoaji wa vifaa vya wazazi kujifungulia inashindwa.

Ametolea mfano katika Kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba ambapo Chadema imeshinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa wameamua kununua vifaa vya kusaidia wakina

mama wakati wakujifungua.

Rwamlaza pia ameitaka serikali kulipa madeni ambayo wanadaiwa na Bohari Kuu ya Madawa (MSD), akisema ni aibu kwa serikali kuendelea kudaiwa na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii.

Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema), yeye amehoji ni kwanini utaratibu wa utoaji elimu katika vyuo vikuu ya Kampala (KIU), IMTU, Muhimbili na Mtakatifu John ni wakibaguzi  kutokana na kila chuo kujipangia idadi ya masomo kwa watu wa kozi moja. 

Pia, Lyimo ameitaka wizara kuhakikisha inaweka bayana ni kwanini watumishi wake waadilifu

wanafunkuzwa kazi pale wanapotoa taarifa kuhusu wizi na ufisadi unaofanywa na watumishi baadhi.

“Yupo mfanyakazi mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la KCMC, amefukuzwa

kazi baada ya kumtumia Rais barua juu ya baadhi ya watu kujiuzia magari ya milioni 100 kwa milioni nane, je hili mnaweza kusema usalama wa watumishi wema ni upi?” amehoja.

error: Content is protected !!