May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge waenda bungeni kwa bodaboda

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Spread the love

IMEBAINIKA kwamba, baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamekuwa wakienda kwenye vikao vya bunge kwa kutumia usafiri wa bodaboda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Job Ndugai, Spika wa Bunge ametoa taarifa hiyo bungeni leo tarehe 16 Aprili 2021, huku akisema, hana tatizo na usafifi huo lakini ni hatari.

“Ni usafiri mzuri na sina shida nao, ila nawaomba kuwa makini,” amesema Spika Ndugai huku akiwakumbusha wabunge hao kwamba, wanapatikana kwa gaharma.

Amewataka wabunge wanaotumia usafiri huo kuwa makini akisisitiza “kupatikana kwenu ni kwa gharama kubwa, nadhani mmenisoma.”

error: Content is protected !!