Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wabunge wacharuka kiingereza kitumike kufundishia ‘tutapigwa goli’
ElimuHabariTangulizi

Wabunge wacharuka kiingereza kitumike kufundishia ‘tutapigwa goli’

Spread the love

MJADALA kuhusu lugha gani itumike kufundishia kati ya kiingereza au Kiswahili umeendelea kutikisa baada ya asilimia kubwa ya wabunge kushauri kuwa kiingereza kitumike kwani Tanzania sio kisiwa.

Pia wameshauri badala ya kulikimbia tatizo la kutokuwa na walimu wenye uweledi wa kufundisha kwa lugha ya kiingereza, walimu hao nao wanolewe ili wapatikane walimu stahiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma… (endelea).

Prof. Ndakidemi

Hayo yamebainishwa leo tarehe 7 Mei, 2022 jijini Dodoma katika Mkutano wa kupokea maoni ya wabunge juu ya maboresho ya sekta ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu ya msingi.

Akichangia maoni katika mkutano huo, Mbunge wa Moshi Vijijini ,Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) amesema Tanzania isipotumia kiingereza watanzania watapata tabu kupata ajira nje ya nchi.

“Kuhusu lugha ya kutumia nitakuwa mkweli, mfano tukisema tunakwenda na kiswahili moja kwa moja ilihali hatutajiandaa kuwa na maneno kamilifu ya kiswahili kwenye sayansi, ukitoka hapa na kiswahili chako ukienda Kenya, Uganda au pengine utabaki hapohapo Tanzania.

Prof. Mkumbo

“Mawazo yangu kuhusu lugha ni kwamba lugha ya kiingereza inatumika duniani kote, hivyo tuipe kipaumbele la sivyo tutakapotoka hapa kwenda kwa wenzetu tutapigwa goli,” amesema.

Amesema Wakenya wanawazidi Watanzania katika sokon la ajira kwa sababu wanajua kiingereza.

“Wakienda huko kwingine wanapewa kipaumbele, kwa hiyo tuhimize kiingereza kitumike na Kiswahili kitumike pale panapostahili,” amesema.

Hoja ya Prof. Ndakidemi imeungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu –CCM, Shari Raymond ambaye amesema watoto wa zama hizi hawaijui lugha mama (lugha za makabila) zaidi ya Kiswahili hivyo ni vema wakafundishwa kwa kutumia kiingereza.

“Bado hatujafikia wakati wa sisi kutumia lugha yetu Kiswahili kufundishia masomo, kiingereza kipewe kipaumbele tena kianze kutumika kuanzia darasa la kwanza,” amesema.

Aidha, Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo (CCM) alipingana na hoja za Prof Ndakidemi pamoja na Shari na kudai kuwa lengo la kumpeleka mtoto shule ni kuboresha maarifa, sio lugha.

“Utafiti niliofanya ni kwamba watoto wetu wanapotoka shule ya msingi wanatoka wakiwa na uelewa lakini wakifika sekondari wanakunja sura.

“Tatizo sio watoto wakajue lugha, tunataka wakapate maarifa, wakienda China wanajifunza kwanza kichina ndipo wajifunze udaktari, Urusi na Japan vilevile, tuondoe boriti kwamba kiswahili ni lugha masikini…tuweke watalaam, watafsiri misamiati ya kisayansi,” amesema.

Wakati Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo kwa upande wake ametolea mifano nchi za Asia kama vile Singapore kuwa inatumia kiingereza na kufanikiwa kukua kiuchumi.

Amesema badala ya kulikimbia tatizo ni vema kulitibu kwa maana kuwa kama hakuna walimu wa kingereza, wafundishwe na kupatikana walimu stahiki wa kufundisha lugha hiyo.

Hata hivyo, alienda mbali zaidi na kuishauri Serikali iondoe kodi kwa wamiliki wa shule binafsi ili wajitokeze wengi kufungua shule nyingi na kupunguza uhaba wa ajira za walimu nchini.

Awali akifungua mkutano huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda leo Jumamosi amesema hadi kufikia Disemba mwaka huu atahakikisha rasimu ya maboresho ya sera na mitaala yake imepatikana wakati kufikia Januari mwaka 2023 wataanza mchakato wa kupata idhini serikalini.

Prof. Mkenda

Amesema kwa vyovyote dunia ina msukumo wa mageuzi ya elimu ndio maana Shirika la Fedha Duniani (IMF) linataka kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa nchi zinazofanya mageuzi kwenye elimu.

Vilevile katika mkutano wa wadai wa elimu uliofanyika hivi karibuni Doha nchini Quatar umeonesha kuwa kuwa kutakuwa na msamaha wa madeni kwa nchi ambazo zitakuwa na mageuzi makubwa ya elimu.

“Kwa vyovyote vile mageuzi ambayo tunakwenda nayo yatakuwa makubwa katika historia ya nchi yetu hatutaki kubahatisha, kukurupuka ndio maana tunahitaji sana kusikiliza maoni yenu wabunge,” amesema Prof. Mkenda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!