Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari Wabunge wachachamaa mgawo ajira watumishi wa afya
Habari

Wabunge wachachamaa mgawo ajira watumishi wa afya

Spread the love

 

BAADHI ya wabunge wameibana Serikali kuhusu mgawo wa ajira mpya za watumishi wa umma wa kada ya afya, katika maeneo yenye upungufu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Leo Jumanne, tarehe 28 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma, wabunge hao wameihoji Serikali kama maeneo yao ni wanufaika wa mgawo hao, ikiwa ni siku mbili tangu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa, kutangaza majina ya watu waliopata ajira kada ya afya zaidi ya 6,000.

Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota, aliihoji lini Serikali itapeleka watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mkoani Mtwara, ikiwemo daktari bingwa.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amejibu akisema hospitali hiyo ilizinduliwa novemba 2021, ikiwa na watumishi 45, na kwamba kwenye ajira mpya imepangiwa watumishi 112 na kwamba ifikapo Julai itakuwa na watumishi 157, wakiwemo madktari bingwa nane.

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa

Naye Mbunge wa Mwibara, Charles Kajege, alihoji “katika mgawo wa watumishi wa kada ya afya ambao umefanyika juzi, nimeona bado katika vituo vyangu vya afya vitatu havikupata. Nini msimamo wa Serikali kuhusiana na upungufu huo.”

Dk. Mollel alimjibu akisema “Waziri wa TAMISEMI alisema kuna nafasi zaidi ya 700 bado hazijapata watu, lakini kwenye wizara ya afya zitabaki. Atashirikiana na waziri wa afya na TAMISEMI kuja kuona namna ya kuziba pengo.

Kwa upande wake Mbunge Viti Maalum, Maimuna Mtanda, amesema Halmashauri ya Newala ina uhitaji wa watumishi wa afya 624, waliopo ni 119 na kwamba katika mgawo wa hivi karibuni ilipata watumishi 38 na kuwa upungufu bado upo. Amehoji lini Serikali itazipa pengo hilo.

Dk. Mollel amemjibu Mtanda akisema, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika maeneo yenye upungufu huo kadiri bajeti itakavyoruhusu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!